Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea
na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona
namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw.
Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa
kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu
ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili
kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania
na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na
baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka
1978. NHC iliiomba Halmashauri ya Wilaya
ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua
viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu
ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu
ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akimpa
maelezo Mjumbe wa Bodi ya NHC Bi Subira Mchumo ya juhudi zinazofanywa na NHC katika Halmashauri
mbalimbali za Wilaya nchini za kuwapatia wananchi makazi bora. Ujumbe huo
ulitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua
mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba na kusisitiza matumizi ya malighafi
zinazopatikana katika maeneo husika ili kupunguza gharama za nyumba hizo.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu
ukikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Wilaya ya Muleba
kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho ya
ukamilishaji.
Msanifu wa Majengo wa NHC Bw. Kintu akitoa maelezo kwa Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ya jengo linalojengwa na NHC eneo la
Mtukula ili kukuza biashara upande wa Tanzania.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ulipata pia fursa ya
kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kujionea juhudi zinazofanywa na
mwekezaji wa kiwanda hicho katika kutoa ajira kwa watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akipewa
maelezo na Kiongozi wa kikundi cha vijana kilichoko Wilaya ya Bukoba Mjini waliyofadhiliwa
na NHC mashine za kutengezea matofali ili kujipatia ajira
No comments:
Post a Comment