Na Magreth Magosso,Kigoma
BARAZA la madiwani halmashauri ya wilaya ya kigoma Mkoa wa
Kigoma,wameadhimia kwenda Bungeni mkoani Dodoma kuonana na Waziri wa Ujenzi
,ili kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Chankele,Mwamgongo Kagunga kwa
nia ya kuondokana na changamoto ya usafiri wa ziwani( Ziwa Tanganyika ).
Azimio hilo limetokana na sintofahamu ya ukamilishwaji wa
barabara hiyo yenye urefu wa km 65 ambapo kupitia bajeti ya mwaka
2013/14 walitumia kiasi cha sh.milioni 194 kukarabati km 20 kutoka mwandiga
,chankele na kushindwa kufika mwamgongo,ambapo wakazi wa ukanda wa ziwa Tanganyika wanatabika na
usafiri wa majini usiokidhi viwango vya usafiri huo.
Awali diwani wa kata ya mwamgongo Kasim Nyamkunga alihoji
baraza uhalali wa barabara hiyo kucheleshwa ujenzi wake,ilihali Rais Jakaya Kikwete na Waziri mkuu Mizengo
Pinda waliahidi kujengwa kwake kabla ya mwaka huu,ambapo wameona adha
ya wakazi wa vijiji vya kagunga,mgambazi,kaziba kuwa,wana tija ya mradi na
waziri Pinda kudai atachangia sh.milioni 300.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi na mazingira Habibu
Hebeye alisema sheria mpya ya mikataba ya miradi ya ujenzi wa miundombinu
inachangia uzoreteshaji wa miradi mbalimbali wa huduma za kijamii kwa kuwa mradi unaoanzia kiasi cha
milioni 50 katika halmashauri zote nchini lazima mkataba upitiwe na mwanasheria mkuu kitendo
kinachokwamisha tija kwa wakati.
Akijibia hilo
Mwenyekiti wa halmashauri Hamis Betese alisema
Februari,10,2015 akishirikiana na mkuu wa wilaya,na mwakilishi kutoka
Tanroada watapanda bungeni kuonana na waziri wa ujenzi ili kukamilisha
mchakato wa ujenzi huo kwa kushirikiana na Tanroad kutokana na
halmashauri
kushindwa kukidhi hitaji la mradi husika.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya Ramadhan Maneno aliwaonya
wataalam wa humo,waache uongo katika usimamiaji wa miradi mbalimbali ya
wananchi,kutokana na baadhi ya watalam kutoa tarifa za uongo hasa katika ujenzi
wa mradi wa maabara ,ambao unasuasua baada ya serikali kuu kuongeza muda wa
miezi sita ili kila halmashauri ifanikishe hilo.
Ally Kisala ni mfanyabiashara mkongwe wa vitenge alisema
kufunguka kwa barabara hiyo ni fursa kwa wananchi kujimiarisha kiuchumi na
shughuli za kitalii kwa kuwa hifadhi ya gombe ipo mwambao mwa ziwa husika na
jamii kupata huduma ya afya kwa wakati kuliko usafiri wa majini ni hatari kwa wajawazito na watoto.
Aidha Katibu wa ccm wilaya hiyo Mobutu Malima alisema changamoto
za wananchi wa ukanda wa mwambao utakwisha kwa ushirikiano baina ya jamii na
viongozi wa serikali ya mkoa haina budi kushinikiza mradi huo uwe chini ya
Tanroad ili kuwakwamua umma kiuchumi,afya na elimu.
No comments:
Post a Comment