Pages

KAPIPI TV

Tuesday, January 20, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Katika ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR) 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati alipowasili katika kijiji cha Dunga jimbo la Uzini mkoa wa Unguja Kusini leo. 3Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano wa ndani pamoja na wawakilishi wenzake wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga. 4 Ndugu Sauda Mpambalyoto Katibu wa CCM wilaya ya Kati mkoa wa Unguja Kusini akisoma taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga leo. 5Kutoka kulia ni Balozi Ali Karume na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakiwa katika mkutano huo. 6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Unguja kusini. 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Vuai Ali Vuai kumwaga zenge la linta kwenye jengo la CCM Dunga. 
 8 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la viungo la Alis Spices &Fruits Farm wakati alipokagua shughuli zinazofanywa katika shamba hilo lililopo Kwabani jimbo la Koani Zanzibar. 14Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miche ya mikarafuu. 15Mmiliki wa shamba hilo Bw. Ali akizingumza na kumshukuru katibu mkuu wa CC kwa kutembelea shamba hilo. 16Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na mmiliki wa shamba hili pamoja na wafanyakazi. 17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye tanki la maji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo kijiji cha Michui jimbo la Koani Zanzibar. 19Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni jimbo la Uzini. 20Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao kuashiria kuiunga mkono na kuipitisha Katiba mpya iliyopendekezwa. 21Mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa jimbo la Uzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni. 22 23Baadhi ya wawakilishi wa timu mbalimbali wakiwa na jenzi zao zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib. 24Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Tunduni wakati wa mkutano wa hadhara, 25Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana wa pili kutoka kushoto akiwa na wawakilishi wenzake wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kijiji cha Tunduni.26Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.

Monday, January 19, 2015

MADIWANI WA HALMASHAURI YA NSIMBO WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO


unnamed1
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mohamed Asenga Akifungua kikao cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki ,kulia kwake ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Slivester Nswima na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Said Juma Maraba.
unnamed2
Wataalam wakifuatilia kwa umakini mjadala wa  kikao cha madiwani Halmashauri ya Nsimbo
(Picha na Kibada Ernest-Katavi)
 
Na Kibada Kibada –Katavi
Madiwani  wa  Halmashauri ya Nsimbo   Wilaya ya Mlele  Mkoa wa   Katavi   wameshauriwa kupima Afya zao na hasa  maambukizi ya VVU  kabla ya kuchukua fomu za kugombea Udiwani kwenye Kata zao  ili waweze  waweze kuwa mfano kwa watu wanaowaongoza na kutambua afya zao   kama kweli watakuwa na nguvu za kutosha kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa kipindi cha kuwepo madarakani.
 
Diwani  wa Kata ya Kapalala  Reward Sichone alitowa ushauri huo   kwenye kikao cha Baraza la Madiwani   Halmashauri ya Nsimbo  baada ya kuwasilishwa kwa  taarifa ya kamati ya kuthibiti ukimwi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Silvester Nswima.
 
 Diwani Sichone alieleza kuwa ni  vizuri kwa madiwani  hasa wa Halmashauri  ya wilaya ya Nsimbo wanao tarajiwa kumaliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa utaratibu na Halmashauri  wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza muda wao wa uongozi mwaka huu ili waweze kuwa mfano kwa watu wao wanao waongoza.
 
 Alilieleza Baraza hilo la  madiwani kuwa  endapo  watapimwa afya zao  mapema  itawafanya wajitathimini  kabla ya kuchukua fomu za kugombea  udiwani.
 
 Sichone alisema  endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye  afya yake  itamsadia  kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya kazi za wananchi  kwenye eneo lake.   
 
Alifafanulia kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambaye atapimwa na kukutwa  na maambukizi ya VVU  halafu  achukue fomu za kugombea tena wakati anajua kuwa hana nguvu za kufanya kazi za wananchi wake   hivyo swala la madiwani kupima  afya zao ni jambo la msingi sana
 
“Jamani mnacke lakini mambo haya ni muhimu sana katika jamii zetu hasa wananchi tunaowaongoza wakiona tunafanya namna hiyo wanakuwa na imani nasisi ingawa kupima siyo lazima ni hiari ya mtu “alisema Diwani Sichone.
 
 Kwa upande  wake Mwenyekiti  wa Kamati ya kudhibiti  Ukimwi  wa Baraza  la Madiwani  Sylvester Nswima  ambae ni Diwani wa Kata ya Sitalike alipinga  ushauri huo wa Diwani Sichone
 
Nswima alieleza kuwa  swala la Madiwani  kupimwa afya zao kwa pamoja  haiwezekani kwani kupima ni  hiyari ya kila mtu na sio lazima,hivyo kila mtu atapima kwa muda wake na kwa hiari yake.
 
Naye Mwenyekti wa  Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alisema   kitendo cha  madiwani kupima afya zao  kinaweza kuwa  ni mfano mzuri kwa watumishi  na wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo kuona viongozi wao wakimwa afya   na kuwafanya nao wataiga mfano wa kupima mara kwa mara afya zao.
 
 Aliwatoa wasiwasi kwa kusema kuwa “Madiwani tusihofu kupimwa   bali tuangalie utaratibu wa  kuwaita wataalamu waje watupime afya  ili tuwe mfano kwa watu wengine  kwenye Halmashauri yetu  na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake”alisema Mwenyekiti Mohamed Assenga.
 
Katika taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa hiariwalifanikiwa kupima watu 1221 kati ya wanaume 668 na  wanawake ni 551 ambapo kati ya watu hao waliopima waliokutwa na maambukizi walikuwa watu 36 kwa Halmashauri ya Nsimbo.

NHC YAENDESHA KONGAMANO LA KUWAJENGEA UWEZO WA KUSIMAMIA BIASHARA MAMENEJA WA MIKOA NA WATENDAJI WENGINE


Mhadhiri Mwandamizi wa Biashara  wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Profesa Michael Munkumba akitoa mada asubuhi hii, kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akifungua kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki. Akizungumza katika kongamano hilo Maagi amesisitiza kuwa kongamano hilo linakusudia kujenga uwezo wa kiuongozi wa kusimamia mabadiliko ya kiutendaji na hatimaye kuwa Shirika la mfano siyoTanzania tu bali Afrika na Duniani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akifungua kongamano hilo.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
 Washiriki wa kongamano hilo wakisalimiana wakati wakiwasili katika kongamano  hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs.
 Washiriki wa kongamano wakiendelea kufuatilia mada iliyotolewa na nguli wa mada ya mabadiliko katika Shirika, Prof. Munkumba.
 Washiriki wakiendelea kufuatilia mada katika kongamano hilo
 Mameneja wa Mikoa ni sehemu ya wajumbe wa kongamano hilo. kutoka kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John, Meneja wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha na Meneja wa Ilala Bw. Jackson Maagi.
 Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia kwa umakini mada ya Prof. Munkumba
 Mhadhiri Mwandamizi wa Biashara  wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Profesa Michael Munkumba akitoa mada asubuhi hii, kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs Hotel Arusha, kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.

MBUNGE FILIKUNJOMBE ATOA MSAADA WA ZAIDI YA TSH MILIONI 15 UKARABATI WA KANISA LA RC MADUNDA

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akizungumza na  waumini wa kanisa la RC Madunda mara  baada ya  kusaidia kanisa  hilo kiasi cha Tsh milioni 15  za ukarabati wa kanisa na vinanda  viwili  vya kwaya kanisani  hapo
Viongozi  wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge  huyo kwa  msaada wake
Waumini  wa kanisa   hilo  wakifurahia  misaada  ya mbunge  wao
katibu  mwenyezi  wa  wilaya ya  Ludewa Filix Haule  (kushoto ) na mmoja kati ya madereva wa mbunge  Filikunjombe Bw Andondile  wakisogeza  vinanda viwili vya kisasa  kwa mbunge Filikunjombe
Mbunge  Filikunjombe kulia akikabidhi  msaada wa vinanda kwa viongozi wa kwaya  katika  kanisa la RC Madunda
Kiongozi  wa  kwaya kanisani hapo akifurahia  msaada wa vinanda  kulia na mbunge Filikunjombe

Mbunge  Deo Filikunjombe (kushoto) akikabidhi msaada  wa  kinanda  kwa viongozi  wa kwaya kwaya katika  kaniksa  hilo la RC Madunda  leo
Mbunge Filikunjombe kulia akizungumza jambo na  paroko msaidizi  wa Madunda  baada  ya  kutoa mchango wake wa Tsh milioni 15  kwa ajili ya  kukarabati kanisa  mchango ambae kiusalama aliahidi  kuuweka katika akaunti ya  jimbo
Mzee Nkwera  ambae ni mshauri  wa  kisiasa wa  mbunge  Filikunjombe akizungumza kanisani hapo
Bw Mgaya  akimshukuru mbunge Filikunjombe


Na matukiodaimaBlog
MBUNGE wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  amechangia   kiasi cha Tsh milioni  15  kwa  ajili ya  ukarabati wa kanisa la Roman Katoriki parokia ya  Madunda  wilayani  Ludewa pamoja na  kusaidia   vinanda viwili kwa  kwaya  mbili kanisani hapo.
Akikabidhi msaada  huo   leo   mara  baada  ya  ibada  ya  jumapili  mbunge
Filikunjombe alisema  kuwa amefika  kanisani  hapo baada ya kuomba kinada na  kwaya  ya  kanisa  hilo na  hivyo  kutokana na kuwepo kwa kwaya  mbili amelazimika   kutoa msaada  wa vinanda kwa kwaya  zote pamoja na  kusaidia kiasi hicho cha  fedha  kwa ajili ya  ukarabati  wa kanisa  hilo.
Kwani alisema  kuwa kanisa   hilo ni mmoja kati ya makanisa  makongwe
yaliyojengwa  miaka  ya  1980 katika wilaya   hiyo ya  Ludewa na  kuwa kanisa   hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa  wilaya ya  Ludewa hivyo  linahitaji  kufanyiwa  ukarabati  mkubwa  ili  kuendelea kuwafanya  waumini  wa kanisa   hilo  kupata  eneo la kuabudia.
Filikunjombe aliwataka    waamuni hao na  waumini  wa madhehebu mengine  katika
wilaya ya  Ludewa  kuendelea  kumwombea afya njema  ili  kupata  nguvu ya  kuwaletea maendeleo kama  ambavyo  ameendelea  kufanya katika wilaya   hiyo  kama  njia  ya  kuwashukuru  wananchi  wake  kwa kumwamini katika  uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa  kumchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo hilo la  Ludewa .
“Imani ambayo  wenzangu  wananchi wa Ludewa  mlioionyesha  mwaka  2010 katika
uchaguzi mkuu  kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe  sitaacha kuwakumbuka   wananchi  wangu  wa Ludewa  kila ninapokuwa bungeni mawazo yangu  kurejesha  ahsante  yangu kwangu na  kuona   wilaya  yetu ya  Ludewa  inaendelea   kupiga  hatua”
Pia mbunge huyo  alisema  kwa  sasa  mkakati  wake na  wa  serikali ya
Rais Dr  Jakaya  Kikwete  ni  kuona  ujenzi wa barabara  ya  lami kutoka Njombe hadi  Ludewa  inajengwa  na tayari  wakandarasi  wa kuanza  ujenzi  huo   wamekwisha  patikana ndani ya  miaka hii miwili bararabara    hiyo  itakuwa  imejengwa na ujenzi  wake  utafanyika kwa awamu  tofauti.
Hata hivyo  alisema  kuwa akiwa mbunge  wa  jimbo  hilo kamwe  hatakubali kuona   wana Ludewa   anawapelekea  maendeleo kwa upendeleo na  kuwa lazima  pande zote  ikiwemo la milimani  , mwambao wote  wananufaika na matunda  yake  kwa  kuwa na maendeleo  wote.
Kwa  upande  wake  katibu  wa itikadi  na uenezi  wa  mkoa  wa Njombe  Honoratus Mgaya  akimpongeza  mbunge    huyo kwa  kuendelea   kusukuma  mbele  maendeleo ya  jimbo  hilo ,alisema  kuwa kazi zinazofanywa  na mbunge  huyo  zimekipatia  heshima chama  cha mapinduzi (CCM) na  kuwa  utendaji mzuri  wa kazi wa mbunge  huyo ndio ambao umeitangaza wilaya ya  Ludewa .

UKAWA WAFICHUA SIRI YA USHINDI MKUBWA SERIKALI ZA MITAA