Kaimu
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa,
Felix Maagi akifungua kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji
wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, kongamano
linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba
zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano
hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja,
misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika
sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki. Akizungumza katika
kongamano hilo Maagi amesisitiza kuwa kongamano hilo linakusudia kujenga
uwezo wa kiuongozi wa kusimamia mabadiliko ya kiutendaji na hatimaye
kuwa Shirika la mfano siyoTanzania tu bali Afrika na Duniani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akifungua kongamano hilo.
Washiriki
mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika
hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Washiriki
wa kongamano hilo wakisalimiana wakati wakiwasili katika kongamano
hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs.
Washiriki wa kongamano wakiendelea kufuatilia mada iliyotolewa na nguli wa mada ya mabadiliko katika Shirika, Prof. Munkumba.
Washiriki wakiendelea kufuatilia mada katika kongamano hilo
Mameneja
wa Mikoa ni sehemu ya wajumbe wa kongamano hilo. kutoka kushoto ni
Meneja wa Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John, Meneja wa Shinyanga Bw.
Ramadhani Macha na Meneja wa Ilala Bw. Jackson Maagi.
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia kwa umakini mada ya Prof. Munkumba
Mhadhiri
Mwandamizi wa Biashara wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini
mwa Afrika (ESAMI), Profesa Michael Munkumba akitoa mada asubuhi hii,
kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika
katika hoteli ya Naura Springs Hotel Arusha, kongamano linakusudia
kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa
na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada
mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya
uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya
usimamizi na uendelezaji wa Miliki.


No comments:
Post a Comment