Pages

KAPIPI TV

Tuesday, September 30, 2014

KINANA ATINGA BUMBULI, ANG'AKA KIWANDA CHA CHAI KUFA MPONDE, ATAKA VIONGOZI WALIOHUSIKA WAWAJIBISHWE.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika kata ya Mponde, akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, leo, Septemba 29, 2014.

      Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Kijiji cha Mponde, Kinana ameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kiwanda cha Chai cha Mponde, kufa baada ya kubinafsishwa kwa njia zinazoashiria kutofuata utaratibu unaotakiwa.
     Pia Kinana ameahidi kulifikisha suala hilo katika vikao vikubwa ikiwemo cha Kamati Kuu ya CCM, ili kuhakikisha unapatikana ufumbuzi wa kero hiyo ikiwemo kuwachukulia hatua viongozi waliohusika.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili katika kijiji cha Mbuzii kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Mbuzii, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, leo Septemba 29, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadili kwa makini jambo na Mbunge wa Bumbuli, Waziri Januari Makamba, wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimboni humo, leo, Septemba 29, 2014.
 Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba akizungumza wakati wa makaribisho ya katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM, Kata ya Mbuzii jimboni humo mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014. pamoja naye ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akizungumza wakati wa makaribisho ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Wapili kushoto), kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, katika jimbo la Bumbumuli, Lushoto mkoani Tanga leo Septemba 29, 2014. Watatu kushoto  ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba.
 Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana eneo la Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, linalojengwa pamoja na ukarabati wa ofisi ya zamani ya Chama ambayo ilikuwa imechakaa kutokana na kuwa ya muda wa miaka mingi tangu enzi za Tanzania kupata Uhuru
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, leo Septemba 29, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na kukagua uhai wa Chama katika jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoa wa Tanga. Kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba akifanya 'kibarua' cha kumpa tofali Kinana..
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zamani la Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii ambalo linafanyiwa upanuzi na ukarabati, alipofika kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo, leo katika jimbo la Bumbuli mkoani Tanga. Nyuma yake ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba
 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrah,man Kinana akisalimiana na Mzee aliyesema kwamba amewahi kuwa dereva wa wakoloni, alipokutana na Kinana aliyewasili kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimbo la Lushoto mkoa wa Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi fungua na hati za pikipiki, kiongozi wa madereva wa Bodaboda katika kijiji cha Dule B, Kata ya Mbuzii wilyani Lushoto mkoa wa Tanga. Pikipiki hiyo imetolewa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwatazama Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba wakiendesha pikipiki za waendesha bodaboda wa Kijiji cha Dule B, Kata ya Mbuzii, katika jimbo hilo wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mganga akiendesha boda boda wakati msafara ukienda kwenye uzinduzi wa shina la wajasiriamali la Maisha Plus kata ya Dule.
 Gari la Maofisa wa CCM na Waandishi wa habai walioko kwenye msafara wa katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana likiwa limevunjika kioo baada ya gari hilo kukwaruzana na lingine, wakati msafara ulipowasili katika Kijiji cha Dule B, kuzindua shina la wakereketwa wa CCM ambao ni wajasriamali wa mradi wa kufyatua matofali wa Kikundi cha Maisha Plus. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana .
 Wakazi wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika kata ya Dule B
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye kambi ya Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila muwa, Maisha Plus
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuelekeza  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba namna ya kupiga randa  kwenye Kituo hicho cha Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya CCM  kuzindua shina la wakereketwa Wajasriamali wa CCM Kikundi cha Maisha Plus, eneo la Dule B ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto.
 Maisha Plus Bumbuli.
 Abdulkarim Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mponde.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.
 Mamia ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika Kata ya Mponde, jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo wa Kinana
 Baadhi ya watu wakiwa wamekaa ,kilimani kuhakikisha wanamuona Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipohutubia Mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde kwenye jimbo la Bumbuli mkoani Tanga leo.
 Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba akieleza kero kuhusu zao la chai na kufa kwa kiwanda cha Chai cha Mponde, alipokaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akuzungumza na wapigakura wake.
Mwananchi wa Mponde akieleza kwa hisia, jinsi wananchi wa Bumbuli wanavyosumbuliwa na kero ya kufa kiwanda cha Chai kilichopo Kata ya Mponde kwa miaka mingi sasa. Asilimia kubwa ya wakazi wa Bumbuli ni wakulima wa Chai.

Monday, September 29, 2014

BODABODA ANAYEKWAPUA SIMU ZA MKONONI NA MIKOBA YA WANAWAKE ANASWA NA POLISI TABORA

Baadhi ya mikoba iliyoporwa na kijana mmoja ambaye ni dereva wa Bodaboda anayeishi kata ya Isevya manispaa ya Tabora aliyefahamika kwa jina moja la BONGE,kijana huyo amekuwa akisumbua sana majira ya kuanzia saa moja usiku kwa kukwapua vitu mbalimbali vya thamani ikiwemo simu za mkononi na mikoba ambapo waathirika wakubwa na matukio ya uporaji yanayofanywa na kijana huyo ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa Tabora mjini.
Baadhi ya vitambulisho zikiwemo kadi za benki mbalimbali zinazodaiwa kuporwa na kijana huyo ambaye hutumia usafiri wa pikipiki kufanyia matukio hayo ya uporaji wa nguvu na kutokomea kusikojulikana lakini hatimaye za Mwizi arobaini,Askari wa jeshi la polisi wamefanikiwa kumkamata na baada ya kumpekua chumbani kwake walikuta vitu hivyo vinavyoonekana pichani.


MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTUMIA REDIO JAMII KUELIMISHA UMMA


DSC_0009
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza  Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano  wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki  mjini Sengerema.

Beatrice alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.

Alisema uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
DSC_0013
Meza kuu: Kutoka kushoto ni Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko, Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Mwenyekiti wa Warsha hiyo kutoka Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara, Bw.Baraka Ole Maika (katikati), Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia).

Uelewa huo upo katika sheria za uchaguzi, gharama na kuona wajibu wao wa kumsaidia Msajili wa Vyama vya Siasa kukabiliana na mazingira hatarishi ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Alisema ni kazi ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria ya vyama namba tano ya mwaka 1992 ya kusajili vyama na kuviangalia na ile ya namba sita ya mnwaka 2010 ambayo inagusia gharama za uchaguzi.

Mratibu huiyo amesema kwamba timu kutoka Ofisi ya Msajili itafika kwenye redio hizo za jamii na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wao katika siasa na kuimariuka kwa demokrasia.

Aidha elimu hiyo inatarajiwa kuwasaidia wananchi kutambua kwamba wana wajibu katika kuhakikisha kwamba menejimenti za uchaguzi zinawajibika pamoja na muuingiliano wake ili kuwa na michakato salama ya cuhaguzi na uchaguzi wenyewe.
DSC_0081
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma. 

Naye Afisa mfawidhi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Ludovick Ringia akizungumzia sheria mbili za vyama vya siasa  alisema kwamba ni wajibu wao kuwaeleza wananchi kuhusu maadili na kanuni katika sheria zinazogusa ukuzaji wa amani katika duru za siasa na demokrasia.
Alisema mradi huo wa kuelimisha wananchi ambao unafanyika kwa udhamini wa Unesco  kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ni moja ya njia za kufanikisha amani  katika kipindi chote kuanzia uchaguzi wa mwisho hadi mwingine.
Alisema wanatumia redio za jamii kwa kuwa redio za kibiashara zimekuwa kikwazo hasa bajeti inapouma kidogo.
Alisema mradi huo ambao unafanyika kwa mwaka mmoja ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo za kuliwezesha taifa kuendelea kuwa na utulivu.
DSC_0073
fisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia), akielezea uwezo wa redio za jamii zinavyoweza kufikia jamii kubwa zaidi nchini wakati ujumbe kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ulipofanya mazungumzo na Wenyeviti wa Bodi na Mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na shirika maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO iliyofanyika kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.

Wenyeviti wa bodi na mameneja hao katika warsha hiyo walielemishwa uboreshaji wa masoko na umuhimu wa redio za jamii juu ya matumizi ya Tehama kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na kushirikisha zaidi wananchi.

Aidha Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Al Amin Yusuph  akizungumzia mafunzo hayo alisema kwamba  mradi huo umekuja wakati muafaka ili kutoa elimu kwa umma, kwani kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa takribani asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini wanasikiliza redio huku asilimia 5 tu ndio wanaangalia runinga.
DSC_0119
Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia) akielezea ufanyaji kazi wa sheria mbili za vyama vya siasa kwa wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini wakati wa warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na SIDA na kuratibu na UNESCO ambayo imefanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0034
Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko akiwasilimia wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini (hawapo pichani).
DSC_0135
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akihoji swali kwa ujumbe uliotoka kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.
DSC_0126
Pichani juu na chini ni baadhi ya wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyomalizika mwishoni mwa juma kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza kwa ufadhili wa SIDA na uratibu wa UNESCO.
DSC_0085

HAFLA YA KUCHANGIA MFUKO WA BONNAH EDUCATION TRUST FUND JIJINI DAR

Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund, Bonnah Kaluwa akitoa hotuba yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.(Picha zote na Othman Michuzi).
 Katibu wa Bonnah Education Trust Fund, Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
25
Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg.Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15 kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund, Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 9.8 kutoka kwa Meneja Uajiri wa Kampuni ya Aramex Tanzania,Jane Stella Njagi (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akiendelea kutoa hotuba yake.
 Meza Kuu.
 Mshehereshaji katika hafla hiyo,alikuwa si mwingine bali Mdau Ephrahim Kibonde.
Baadhi ya wageni waliohudhulia hafla ya ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund wakifatilia kwa makini harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.