Pages

KAPIPI TV

Monday, September 29, 2014

BODABODA ANAYEKWAPUA SIMU ZA MKONONI NA MIKOBA YA WANAWAKE ANASWA NA POLISI TABORA

Baadhi ya mikoba iliyoporwa na kijana mmoja ambaye ni dereva wa Bodaboda anayeishi kata ya Isevya manispaa ya Tabora aliyefahamika kwa jina moja la BONGE,kijana huyo amekuwa akisumbua sana majira ya kuanzia saa moja usiku kwa kukwapua vitu mbalimbali vya thamani ikiwemo simu za mkononi na mikoba ambapo waathirika wakubwa na matukio ya uporaji yanayofanywa na kijana huyo ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa Tabora mjini.
Baadhi ya vitambulisho zikiwemo kadi za benki mbalimbali zinazodaiwa kuporwa na kijana huyo ambaye hutumia usafiri wa pikipiki kufanyia matukio hayo ya uporaji wa nguvu na kutokomea kusikojulikana lakini hatimaye za Mwizi arobaini,Askari wa jeshi la polisi wamefanikiwa kumkamata na baada ya kumpekua chumbani kwake walikuta vitu hivyo vinavyoonekana pichani.


No comments: