Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 2, 2015

BOSS WA UN, ALVARO RODRIGUEZ ATEMBELEA SABASABA, ASEMA MAONYESHO NI FURSA YA KUJIFUNZA

IMG_5941
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_5945
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati wakielekea katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lilipo Karume Hall mara tu baada ya kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi na mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa dunia sasa imekuwa kijiji kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo unakusudia kuendelea kuwepo kushirikiana na watanzania katika kutatua matatizo kwenye Nyanja mbalimbali.
Bw. Alvaro amewataka watanzania kusherehekea pamoja miaka 78 ya Umoja hapa nchini kwa kutoa maoni mbali mbali na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Amesema kwa pamoja tunahitaji kuzungumzia usawa wa kijinsia, masuala ya kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mambo ya kiuchumi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa kufanya juhudi za kusaidia vijana kuanzia ngazi za chini kabisa na kuwawezesha kuwa wajasiriamali.
Amesema kitendo cha Umoja huo kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba sambamba na kijana Amos Mtambala waliyemuwezesha kwa kumpatia mafunzo ya sanaa za uchoraji kumeleta hamasa kubwa miongoni mwa vijana wasio na ajira nchini.
IMG_6027
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_6032
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5959
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, akitoa maelezo jinsi wanavyoelimisha wananchi kuhusiana shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini sambamba na malengo ya millenia yanayofikia kileleni kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5962
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akielezea maeneo ya Program mbalimbali za UNDAP yaliyofanikiwa nchini Tanzania kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko.
IMG_5965
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akikabidhi taarifa ya mwaka ya UNDAP kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (katikati) aliyefuatana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) walipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall.
IMG_5973
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akitoa maelezo jinsi alivyowezeshwa kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5981
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini, Magnus Minja akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuhusiana na program ya kazi njenje ya mradi wa kufundisha vijana katika shughuli za ujasiriamali inayoratibiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambapo kijana Amos iliweze kumuinua na kujiajiri kupitia sanaa ya uchoraji.
IMG_5995
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya karatasi inayotoa maelezo ya jinsi ya Watanzania wanavyoweza kushiriki kutoa maoni mbalimbali juu ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kutuma SMS ambayo ni bure bila malipo yoyote na moja kwa moja kumfikia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
IMG_6021
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na waaandishi wa habari katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa ambao wanashiriki maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_6038
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko mfuko wenye machapisho na vijarida mbalimbali vya Umoja wa Mataifa.
IMG_6467
Afisa Utawala wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Magoma (wa pili kushoto) akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na Wa pili kulia ni Mchumi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vainess Molle.
IMG_6476
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akijibu swali la Bw. Suleiman.
IMG_6494
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akionyesha namna ya kutoa maoni ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya SMS ambayo ni bure kwa mitandao yote ya simu za mkononi nchini kwa wadau waliotembela banda la UN Tanzania.
IMG_6435
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez ajibu maswali mbalimbali yalitumwa kwa njia ya mtandao na wananchi katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_5997
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_6456
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja na Mkuu wa UN Tanzania.

NI MSIBA TENA JAMBO CONCEPTS (T) LTD, WACHAPISHAJI WA GAZETI LA JAMBO LEO


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Jambo Concepts (T) Ltd, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti na Jarida la Jambo Brand, limempoteza mfanyakazi wake mwingine wa idara ya masoko, Kinai Mtinda (pichani), baada ya kufariki dunia saa 7 usiku wa kuamukia leo katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach na taratibu zingine kuhusiana na msiba huo zitatolewa baadae.

Marehemu Kinai ameacha watoto wawili.

Kifo cha Mtinda kinakuja ikiwa ni siku chache tangu afariki dunia Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Ramadhani Kibanike mwishoni mwa mwezi uliopita. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe Amina.


AIRTEL SMARTFONIKA YAMFIKIA MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS TV


 Ofisa Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya kisasa mapema wiki hii katika duka la  wazi la Airtel lililopo Game Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
 Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.
 Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani City.
 Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
 Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
 Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
  Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu huo.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo mkubwa.

"Tumejipanga vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.

Mmbando alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mmbando ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wa Airtel kutembelea banda lao lililopo katika viwanja hivyo ili kupata huduma mbalimbali pamoja na kujipatia simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

ELUMELU CALLS FOR AN END TO ENERGY POVERTY

Pix 1
L-R: Former president of Ghana John Kufuor; President of Cote D'Ivoire Alassane Ouattara, Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG); Tony O. Elumelu, Chairman of Heirs Holdings and Co-Chair of the AELG; Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan yesterday to discuss regional solutions to the electricity deficit in Africa.
Pix 2
L-R: Former presidents of Nigeria and Ghana Olusegun Obasanjo; John Kufuor; President of Cote D'Ivoire Alassane Ouattara, Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG); Tony O. Elumelu, Chairman of Heirs Holdings and Co-Chair of the AELG); Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan yesterday to discuss regional solutions to the electricity deficit in Africa.
Pix 3
Energy For ALL: l-r. Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo and Tony O. Elumelu, Chairman of Heirs Holdings and Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG) during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan, Cote D'Ivoire to discuss regional solutions to addressing the electricity deficit in Africa
Pix 4
Energy For ALL: l-r. Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo and Tony O. Elumelu, Chairman of Heirs Holdings and Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG) during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan, Cote D'Ivoire to discuss regional solutions to addressing the electricity deficit in Africa.
Pix 5
L-R: Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG) and Chairman Heirs Holdings, Tony Elumelu, Former presidents of Nigeria and Ghana Olusegun Obasanjo; John Kufuor; President of Cote D'Ivoire Alassane Ouattara, Co-Chair of the AELG; Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo and other African leaders during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan yesterday to discuss regional solutions to the electricity deficit in Africa.
“Providing access to electricity for schools, hospitals, businesses and industries is the single most impactful intervention that can be made to transform the continent. It has tremendous implications for job creation, health, food security, education, technological advancement and overall economic development.” Mr. Tony Elumelu said today in Abidjan.
African businessman and philanthropist Tony Elumelu who is the Chairman of Heirs Holdings and Founder of the Tony Elumelu Foundation joined African economic and political leaders today in Abidjan to call for an end to energy poverty on the continent. The leaders came together in Abidjan under the umbrella of the African Energy Leaders Group (AELG).
The AELG was launched during the 2015 World Economic Forum in Davos, Switzerland. The group brings together political and business leaders at the highest level to drive the reforms and investment needed to end energy poverty and to ensure sustainable fuel supplies on the continent.
Mr. Elumelu is a founding partner and Co-chair of the AELG. Other founding partners of AELG include Ivoirian President Allasane Ouattara; Ghanaian President John Mahama; President, African Development Bank Dr Donald Kaberuka; President & CEO, The Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote; President ECOWAS Commission, Kadre Desire Ouedraogo; and President UEMOA Cheikhe Hadjibou Soumare.
Providing access for all Africans to reliable, affordable energy services and efficient appliances by 2030 is a key goal of AELG. The AELG objective of ensuring universal access to modern energy is in line with those of the United Nations Sustainable Energy for All (SE4All) initiative run by the UN Secretary General's Special Representative Kandeh Yumkella, one of the champions of the AELG. Mr. Elumelu pledged to support the work of AELG.
“I am making a pledge to provide $150,000 over the next three years to support the operations of the AELG secretariat,” he said. “I want to call on the governments of the member states of the ECOWAS region, and AELG members and partners to also step up with significant multi-year commitments to sustain the organization.” Following Mr Elumelu's lead, pop superstar, Akon, who was also in attendance at the event to promote his Lighting Africa Initiative, pledged $200,000 to support the work of the AELG secretariat.
On the closing panel for the AELG meeting where Elumelu was joined by Akon, former presidents Obasanjo and Kufuor, Vice President Osinbajo, and the Prime Ministers of Cote D'Ivoire, Mali, Benin, Togo, and Niger, he challenged the public sector leaders to follow the lessons learned from the democratization of the telecoms sector to unlock growth in the power sector.
In 2013, Tony Elumelu committed to investing $2.5 billion in the power sector in Africa through President Obama's Power Africa Initiative. Transcorp Plc, Chaired by Elumelu, acquired the largest gas powered generating plant in Nigeria, located in Ughelli, Delta State in late 2013. By the end of this year, the Transcorp Ughelli plant will be generating 1,000 MW and the company is in discussions with GE to add an additional 1,000 MW soon after.

AIRTEL YAINGIA MKATABA NA FINCA WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA


 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.
 Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu huduma hiyo. Kulia ni Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.

Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa.






 Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa akizungumza katika mkutano huo. 

 Maofisa wa Airtel na Finca wakionesha bango wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benji ya Finca Microfinance kwaajili ya kuwezesha wateja kuzifikia pesa zao kirahisi kwa kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hiyo mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoa kwenye simu kwenda benki.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha wateza wao kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalam azaidi.

Alisema kwa kutambua finca sasa ni taasisi ya kibenki wameona ni vyema kuungana na kuweza kutoa huduma za kuhamisha pesha kwa usalama na kwa ghalama nafuu kupitia simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima.

"Airtel itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wake kwa kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa wateja," alisema.

Naye Meneja wa Kanda wa Finca Microfinance Benki, Sarah Daffa alisema huduma hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zao.

"Tunawashukulu Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money, tunaimani ushirikiano utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya miamala inayofanyika kwa urahisi na salama," alisema.

"Wateja wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote mahali popote mara nyingi zaidi ikiwa tu watasajiliwa kweye huduma hiyo na akaunti yake ya benki ikiwa hai," alisema.

Wednesday, July 1, 2015

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA MO DEWJIBLOG MAONESHO YA SABASABA LEO

IMG_6278
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisalimiana na Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale alipotembelea katika banda la mtandao huo ambao mwaka huu mwezi Septemba unatimiza miaka 7 tangu kuanzishwa ambapo wametumia fursa ya maonyesho ya saba saba kukutana na wadau mbalimbali wanaotumia mtandao huo kupata habari mbalimbali sambamba na kubadilishana mawazo na ushauri wa maboresho ya kazi. Kushoto aliyefuatana naye ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu. Kulia ni mdau wa karibu na mshauri wa mtandao wa habari Modewjiblog, Lemmy Hipolite.
IMG_6282
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiangalia moja ya documentary ya TV katika banda hilo minayoonyesha wadau mbalimbali wanaotumia mtandao huu ambao walipata kuhojiwa.
DSC_0646
Mmoja wa wadau wa Modewjiblog, Rehema Pascal akiuzungumzia mtandao wa habari wa Modewjiblog alipotembelewa ofisini kwake wakati wa kurekodi 'documentary' hiyo.
IMG_6284
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa kwenye mtandao wa habari wa Modewjiblog alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba yanaoendelea kurindima katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_6297 IMG_6304
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiondoka mara baada ya kutembelea banda la Modewjiblog, lililopo katika banda la MeTL Group.
IMG_5671
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige akitoa maelezo juu ya mtandao huo unavyofanya kazi zake ambapo aliwataka vijana hao kutembelea mara kwa mara ikiwemo kufaidika na nafasi za ajira zinazotolewa kwenye mtandao huo zikiwemo habari za kitaifa na kimataifa, burudani, michezo, utamaduni n.k.
IMG_5688
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (kulia) na Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale wakikabidhi zawadi za fulana maalum kwa wadau waliotembelea katika banda la mtandao huo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba yanaoendelea kurindima katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5508
Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale akikabidhi zawadi ya kofia na fulana kwa Mmiliki wa blog ya Kajunason blog, Cathbert Kajuna (kulia) aliyetembelea banda la mtandao huo.
DSC_1164
Wadau wakiendelea kumiminika kwenye banda la Modewjiblog katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba yanaoendelea kurindima katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0795
Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale akikabidhi zawadi ya fulana na kofia kwa Mwandishi wa Michuzi blog, Chalila Kibuda aliyembelea banda hilo.
DSC_1277
Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale (kulia) akitoa maelezo ya utofauti wa habari za kwenye magazeti na blog kwa mmoja wa wadau anayesoma habari mbalimbali katika mtandao huo, Peter Chilumba.

KAMPUNI YA MABIBO BEER YAIDAI TUME YA USHINDANI (FCC) SH.TIRIONI MOJA

 Bia za Windhoek zinavyoonekana.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira (katikati), akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili, Stephano Kamala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
 Wakili, Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza Kuu. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Mabibo, 
Alice Marco.
 Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mdau Faustine Kapama akiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambayo ni wasambazaji wa bia ya Windhoek inaidai Tume ya Ushindani (FCC), sh.tirioni 1 kwa kukiuka uhalali wa mkataba wa Mabibo na kudai unapingana na ushindani.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT) mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za Windhoek kipekee katika soko la Tanzania.

Hayo yalibainishwa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi ambao ni sawa na kutangaza kuwa mkataba kati ya Mabibo Beer Wines and Spirits na Namibia Breweries Limited uliosajiriwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma wa kipee wa Mabibo haukuwa halali kisheria.

"Si FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya Mahakama za Tanzania" alisema Rugemalira.

Aliongeza kuwa mbali na kuzidisha na kupanua mamlaka yao maamuzi ya FCC na FCT pia yanapuuza ukweli wa msingi. Wakati Windhoek ni bidhaa maalumu inayofahamika kimataifa, ambapo mauzo yake nchini ni kiasi cha asilimia 0.05 tu ya soko la jumla nchini na sio kampuni inayotawala soko la  bia Tanzania.

Alisema Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri isiyo halali ya FCC imeruhusu muendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.

JE,HIVI NI LINI WANANCHI WA KAWAIDA WATAKOMBOLEWA KUONDOKANA NA HALI DUNI YA MAISHA?

Mmoja kati ya wananchi wa mkoa wa Tabora ambao ni miongoni mwa watu wanaotegemea kipato chao kitokane na shughuli mbalimbali ikiwemo ya ukataji mkaa hatua ambayo inaelezwa kuwa inaathiri kwa kiasi kikubwa uharibifu wa rasilimali misitu lakini ni moja ya shughuli zinazowasaidia kuendesha maisha wananchi wa kipato cha chini kama huyu.
Je,hii inaweza kuwa ni safari ya matumaini ya kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini kama huyu ambaye anajishughulisha na ukataji mkaa na kuharibu mazingira ya misitu?


WAZIRI MKUU AHIMIZA WANANCHI KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA KUPIMA AFYA ZAO NA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA

1nh
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na umati wa watu waliokisanyika katika banda la NHIF juu ya umuhimu wa watu kupima afya zao mara kwa mara na kuzingatia kanuni bora za maisha ili kuepuka maginjwa yasiyoambikiza ambayo mengi husababishwa na unene uliokithiri.
2nh
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kuhusu huduma zinazotolewa na banda la NHIF katika Maonesho ya Wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa Mtwara.
nh3
Msururu wa wananchi wa Mtwara wakisubiri zamu zao kupima afya zao wakati Mzee aliyejitokeza kupima akipatiwa huduma.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda leo ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhimiza wananchi kuzingatia afya bora ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama Sukari na Shinikizo la damu. 

  Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu ya huduma zitolewazo katika banda hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando alisema NHIF anaungana na Serikali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhimiza wananchi kupima afya zao na kuishi mtindo bora wa maisha unaozingatia lishe bora na mazoezi. 

Alisema 'Mfuko umejiwekea utaratibu wa kupima afya bure kwa wananchi kila unaposhiriki maonesho mbalimbali ili kuwajengea wananchi tabia hiyo na kuonesha umihimu wa suala hilo ili kuepuka madhara makubwa ya afya na vifo ambavyo vingeweza kuepukika'  

Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mtwara Bi. Joyce Sumbwe alisema tangu maonesho hayo yaaenze tarehe 24 Juni watu 1,800 wameshapimwa afya zao na 32% kati yao wamepatikana na unene uliokithiri ambao ni chanzo kikubwa cha magonjwa hayo.  

Wengi wa wananchi waliojitokeza walionekana kutokujia kuwa wanatembea na shinikizo la damu na walishauriwa kwenda kituo cha afya ili kuanza matibabu.  

Naye Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi. Anjela Mziray alitoa wito kwa wananchi kujiunga na NHIF ili kumudu gharama za matibabu ambazo ziko juu na magonjwa huja bila taarifa hata wakati ambapo mtu hana fedha mfukoni. 

Alisema suluhisho ni kwa wananchi wote kujiunga na Bima ya afya.