Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 1, 2015

WAZIRI MKUU AHIMIZA WANANCHI KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA KUPIMA AFYA ZAO NA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA

1nh
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na umati wa watu waliokisanyika katika banda la NHIF juu ya umuhimu wa watu kupima afya zao mara kwa mara na kuzingatia kanuni bora za maisha ili kuepuka maginjwa yasiyoambikiza ambayo mengi husababishwa na unene uliokithiri.
2nh
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kuhusu huduma zinazotolewa na banda la NHIF katika Maonesho ya Wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa Mtwara.
nh3
Msururu wa wananchi wa Mtwara wakisubiri zamu zao kupima afya zao wakati Mzee aliyejitokeza kupima akipatiwa huduma.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda leo ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhimiza wananchi kuzingatia afya bora ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama Sukari na Shinikizo la damu. 

  Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu ya huduma zitolewazo katika banda hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando alisema NHIF anaungana na Serikali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhimiza wananchi kupima afya zao na kuishi mtindo bora wa maisha unaozingatia lishe bora na mazoezi. 

Alisema 'Mfuko umejiwekea utaratibu wa kupima afya bure kwa wananchi kila unaposhiriki maonesho mbalimbali ili kuwajengea wananchi tabia hiyo na kuonesha umihimu wa suala hilo ili kuepuka madhara makubwa ya afya na vifo ambavyo vingeweza kuepukika'  

Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mtwara Bi. Joyce Sumbwe alisema tangu maonesho hayo yaaenze tarehe 24 Juni watu 1,800 wameshapimwa afya zao na 32% kati yao wamepatikana na unene uliokithiri ambao ni chanzo kikubwa cha magonjwa hayo.  

Wengi wa wananchi waliojitokeza walionekana kutokujia kuwa wanatembea na shinikizo la damu na walishauriwa kwenda kituo cha afya ili kuanza matibabu.  

Naye Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi. Anjela Mziray alitoa wito kwa wananchi kujiunga na NHIF ili kumudu gharama za matibabu ambazo ziko juu na magonjwa huja bila taarifa hata wakati ambapo mtu hana fedha mfukoni. 

Alisema suluhisho ni kwa wananchi wote kujiunga na Bima ya afya.

No comments: