Maandamano
ya sherehe ya kutunukiwa nishani ya heshima ya udaktari Askofu Paulo
Samwel Njoghomi (mwenye miwani) wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida
mjini. Nishani hiyo imetolewa na Chuo kikuu cha Africa Graduate cha
nchini Sierra Leone.
Mkuu
wa chuo kikuu cha Africa Graduate Timoth Kazembe, akimtunuku nishani ya
heshima Askofu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Paulo Samwel Njoghomi
Hafla hiyo ilifanyika katika kanisa la FPCT mjini hapa.
Makamu
Mkuu wa chuo kikuu cha Africa Graduate cha nchini Sierra Leone, Askofu
Profesa, Stephano Nzawa, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya kumtunikia
nishani ya heshima baada ya kubaini utendaji wake uliotawaliwa zaidi na
uaminifu.
Askofu
Dk. Paulo Samwel Njoghomi, akishukuru uongozi wa chuo kikuu cha Africa
Graduate cha nchini Siere Lione,kwa uamuzi wao wa kumtunikia nishani ya
heshima baada ya kubaini utendaji wake uliotawaliwa zaidi na uaminifu.
Mwana
kwaya ya huduma ya kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini
Singida,wakitubuiza kwenye waumini na wakazi wa mkoa wa
Singida,waliohudhuria mahafali ya 20 ya chuo kikuu cha Africa Graduate
nchini Sierra Leone ambapo askofu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini
hapa, Paulo Samwel Njoghomi,alitunikiwa nishani ya heshima na chuo
hicho.
Baadhi
ya waumini na wakazi wa mkoa wa Singida,waliohudhuria mahafali ya 20 ya
chuo kikuu cha Africa Graduate nchini Sierra Leone ambapo Askofu wa
kanisa la Pentekoste (FPCT) mjini hapa, Paulo Samwel
Njoghomi,alitunikiwa nishani ya heshima na chuo hicho.(Picha zote na
Nathaniel Limu).
No comments:
Post a Comment