Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 23, 2015

WATU 120 WAKOSA KUANDIKISHWA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Na Magreth Magosso,Kigoma

WANANCHI  120 wa Kijiji cha Munyogera wilayani Buhigwe Mkoa wa Kigoma,wamekosa fursa ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na uchache wa siku saba walizopewa kufanya hivyo kuliko wingi wa jamii husika.
 
Akizungumza hayo katika  kikao cha Madiwani   cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2014/15 kilichofanyika  juzi katika shule ya msingi Buhigwe  ndipo Diwani wa Kijiji hicho Edson Dungwa alisema pamoja na kijiji hicho kupewa kipaumbele cha kupewa mashine za BVR kwa ajili ya kuandisha wananchi lakini imempa wakati mgumu kwa wakazi hao.
 
Dungwa alisema wananchi  152 wamemfuta nyumbani kwake na kumtaka awasaidie namna ya kufikiwa na huduma ili wafanikishe mchakato wa kuchagua na kuchaguliwa sanjari na kulinda uraia wao,kwa kuwa kijiji chao kipo mpakani na nchi ya Burundi .
 
“nimewandika katika karatasi na kupitia kikao hiki naomba majibu juu ya hatma ya wananchi hawa,ambao wengi ni wakulima wa mashamba ya mbali na ni raia wa hapa,shida ni muda hautoshi “ alisema Diwani huyo.
Akijibia hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe  Saimoni Mbee alisema changamoto hiyo  ina mashaka , halmashauri ni kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo waliongeza siku mbili katika kijiji hicho ili kufidia waliopo mbali .
 
Mbee alibainisha kuwa,watalifanyia kazi karatasi lenye majina ya wakazi hao,kwa kuwa kuna baadhi ya raia wan chi jirani hutumika katika zoezi hilo ambapo kwa siku chache zoezi lianze walishakamatwa watu raia wa huko ambao walinufaika kinyume cha sheria.
 
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya hiyo Mary Tesha aliongeza kwa kusema wanasiasa ni watata,kwa kuwa buhigwe ipo mpakani mwa kigoma hasa kijiji hicho watatumia idara ya uhamiaji ili kuchunguza kwa makini wananchi walioachwa ili kujiridhisha kwa kuwa ni kipindi kigumu kwa wagombea wapo tayari kufanya chochote kukidhi mahitaji yao.

No comments: