Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile (wa pili kulia), akizungumza na wachezaji wa timu za Dubu na Tumaini (hawapo pichani), wakati akifungua mashindano ya kombe la umoja na mshikamano maarufu kama Diwani Cup yaliyoanza uwanja wa Kibamande eneo la Mwasonga Manispaa ya Temeke Dar es Salaam jana. Kulia ni mlezi wa mashindano hayo, Diwani wa Kata ya Kisarawe II, Issa Zahoro.
Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II, Issa Zahoro, akikagua timu ya Dubu kutoka eneo la Mwasonga.Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II, Issa Zahoro, akikagua timu ya Tumaini kutoka katika kata hiyo.
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akiwasalimia mashabiki wakati akiwasili kufungua mashindano hao.
Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.
Wazee wa Kata hiyo wakifuatilia kwa karibu mashindano hayo.
Timu ya Tumaini ikiomba dua kabla ya kuanza mashindano hayo.
Timu ya Tumaini katika picha ya pamoja.
Timu ya Dubu katika picha ya pamoja.
Waamuzi wanaochezesha mashindano hayo.
Timu na waamuzi wakielekea kukaguliwa.
Mchezaji wa timu ya Tumaini, Tamimu Mussa (kushoto), akimtoka Josephat Kalinga wa timu ya Dubu.
Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.
Hapa ni kazi tu uwanjani.
Hapa mchezaji mdogo kuliko wote kutoka timu ya Dubu, Mwishehe Omary akipewa zawadi ya sh.10,000.
Mchezaji aliyeng'ara katika mashindano hayo akipokea zawadi ya sh.10,000.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
MASHINDANO ya kombe la umoja na mshikamano maarufu kama Diwani Cup yamezinduliwa rasmi katika eneo la kisarawe II,kwa timu za dubu kupepetana dhidi ya timu ya Tumaini zote za kata hiyo.
Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Kibamande kilichopo eneo la Mwasonga, Mbunge wa Kigamboni Faustine ndugulile alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Ndugulile
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Ayubu Mkonde aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.
Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II, Issa Zahoro alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa eneo la Kisarawe II.ambapo katika mchezo wa ufunguzi timu ya Dubu ilishindwa kutambiana dhidi ya timu ya Tumaini kwa kutoka uwanjani bila ya kufungana. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment