Na Magreth Magosso,Kigoma
WATU sita wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kigoma
na wengine 36 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma,kwa tuhuma za
kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali ukiwemo
Mkia wa Tembo na Kobe aliye hai kinyume cha sheria husika.
Akifafanua tukio hilo jana mbele ya wandishi wa habari
ofisini kwake kigoma Ujiji Kamanda wa
Polisi Jafari Mohamed alisema kuanzia
5,Januari-25 ,Februari mwaka huu,TANAPA wakishirikiana na Askari polisi katika
doria ya pamoja katika maeneo tete ya ujangili katika wilaya ya Kasulu ,Kibondo
na Kakonko walifanikiwa kukamata nyara kadhaa na kukamata silaha aina ya
Shortgun isiyokuwa na namba,gobore moja sanjari
na risasi 135.
Alisema mbali na hilo Februari 10,2015 saa 11.00 katika
kijiji cha Kibingo kata ya Kizigizi tarafa na wilaya ya kakonko watu wawili akiwemo raia wan chi jirani ya
Burundi Rushao Hamuli(76) na Sebastiani John(44) wote kwa pamoja wamefikishwa
katika mahakama ya wilaya ya kasulu kwa tuhuma za kushikwa na nyara za serikali
za wanyama mbalimbali ikiwemo ngozi ya chui na sungura.
Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakimiliki kobe hai,pembe ya
swala,ngozi ya chatu,mifupa ya chatu,ngozi mbili za pungo,ndege aina ya mwewe
maji mmjoa,kutokana na vielelezo hivyo wamefunguliwa mashtaka yao CC.29/2015.
Katika tukio la pili
mtu mmoja raia wa Burundi Mpawe Ophasabhose(23)
saa 1.00 usiku katika kijiji cha Kibande wilayani Buhigwe alikamatwa na risasi
135 za bunduki ya kivita aina ya G.3 akisaka wateja na anashikiliwa na jeshi la polisi ili kubainisha
mtandao wa uhalifu hasa uuzaji na usambazaji wa silaha na risasi uliozagaa mkoani Kigoma na mikoa jirani.
Aidha Kamanda huyo amewapongeza wananchi kwa kutoa ushirikianao
kupitia ulinzi shirikishi ,ambao umezaaa matunda ya kukamatwa kwa jumla ya watuhumiwa 43 na kuonya wanaomiliki silaha
kinyemela wazirudishe katika ofisi za serikali za mitaa ili kudhibiti biashara haramu ya silaha za moto na ujangili
katika hifadhi za taifa.
No comments:
Post a Comment