Pages

KAPIPI TV

Friday, February 6, 2015

RUSHWA NI TATIZO KUBWA KWA WENYE HALI DUNI - KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

WANANCHI  wa  Kigoma wataka udhibiti wa rushwa katika utoaji wa huduma ya sheria , ili kuwajengea imani wananchi wenye kipato cha chini kupeleka mashtaka yao Mahakamani  na kuhudumiwa bila kuwekewa mazingira ya ukiukwaji wa haki tarajiwa.
 
Wakizungumza na wandishi wa habari kwenye madhimisho ya kilele siku ya sheria nchini Zuwena Shaban na Enosi Magumba kwa nyakati tofauti wakili kuwepo kwa rushwa katika uendeshwaji wa kesi mbalimbali ,ambapo kwa mwananchi mwenye kipato cha chini hushindwa kufika mahakamani kupigania haki husika.

“ucheleweshwaji wa kesi  kuhairishwa kila wakati ni shida kwa maskini kwa kuwa,uchumi hautoshi kufuatilia kesi kwa muda mrefu,mfumo mbovu wa utolewaji wa sheria ni chanzo cha haki kupotea kwa mwenye haki,waliofungwa wengi ni watu wa kawaida katika jamii” walidai wananchi hao.

Naye Mgeni rasmi Ramadhani Maneno kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa hapa alitaka kila mtu atimize wajibu wake kulingana na nyadhifa  kwa kuzingatia weledi ,ili kupunguza malalamiko ya raia kwa Serikali iliyopo madarakani na kupunguza adha zisizohitajika.

Alisema wanasheria wawatumie vikao kupeana mrejesho wa changamoto zinazowakabili katika uwajibikaji sanjari na kuwadhimia wanaokiuka miiko na taratibu za maadili ya taalum,a hiyo,Huku ataka masijala za kuhifadhi majarada ya kesi ziboreshwe ili kuondoa usumbufu kwa walaji.

Kwa upande wa Hakimu Mkazi wilaya ya kigoma Silvester Kahinda akiri rushwa kushamiri katika mahakama nyingi nchini na kudai shida ya kigoma kesi kuzorota inachangiwa  na uhaba wa mahakama za mwanzo ambapo kwa wilaya ya Buhigwe na Kakonko hazina huduma hiyo na kati ya mahakama 33 zinazotoa huduma ni 16  tu.

Aidha mwakilishi wa mawakili wa kujitegemea Danieli Rumanyila alisema sheria ya mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 ,kifungu cha (5) kinasema wafungwa wana haki ya kupata huduma bora za afya,malazi lakini jela nyingi zinawaweka wafungwa katika mazingira hatarishi hasa malazi hulala pachafu ,shuka chafu na hulundikwa mithili ya mizigo.

No comments: