Pages

KAPIPI TV

Friday, February 6, 2015

KIGOMA YAJIPANGA KUDHIBITI UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Na Magreth Magosso,Kigoma

WAKAZI wa Kigoma wametakiwa watumie dawa aina ya ` Safeguard ‘ili kujilinda na  ugonjwa  wa kipindupindu ambao umesababisha zaidi ya watu 185 kupatwa na ugonjwa huo na watano kupoteza maisha.

Ugonjwa huo umeenea kwa kasi mkoani humo hasa katika mwalo wa katonga ,kibirizi hali inayotishia wakazi wa manispaa ya kigoma ,wilaya ya kigoma na kasulu ambapo hadi leo kasulu ina wagonjwa saba na manispaa ya ujiji ina wagonjwa 5.

Akifafanua hilo Mganga mkuu wa Mkoa huo Leonard Subi alisema wananchi hawana budi wabadili tabia kwa kuchemsha maji,kujenga vyoo bora sanjari na kunawa mikono kabla na baada ya kwenda chooni na unapohitaji kula kitu chochote.
 
“chanzo cha ugonjwa huu  ni  chakula kilichochanganyika na kinyesi ,wasiamini maji ya chemichemi na visima vifupi  wachemshe  na tumegawa dawa hiyo katika kila mtaa wa serikali za mtaa na vijiji husika katika wilaya hizo,watsijisaidie vichakani na ziwani ni chanzo cha vimelea husika” alibainisha Dkt.Subi.
 
Aidha aonya wapika vyakula mitaani hususani mama lishe wandae chakula katika mazingira safi na kuhifadhi katioka vifaa bora kwa ajili ya vyakula husika,ili kuepusha gharama kwa Serikali ambapo imeleta maboksi ya waterguard 1203 za maji 160 na vidonge 143.

No comments: