Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda |
Akisimulia tukio hilo la mauaji ya kutisha,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda alisema watu hao ambao ni majambazi walivamia nyumbani kwa Bw.Wilson Masanila(32)huko katika Kitongoji cha Idodomya majira ya saa nane usiku wa mkesha wa krismas kwa nia ya kutaka kupora fedha ambapo walimpiga na kitu chenye ncha kali na hatimaye kupoteza uhai wake.
Kamanda Suzan aliendelea kufafanua kuwa waharifu hao baada ya kumuua Bw.Wilison ambaye ni mfanyabiashara ya ng'ombe,walimfuata msaidizi wake Juma Ujege(34)ambaye alikuwa nyumba ya pili na kumuamuru atoe fedha walizouza ng'ombe wakiwa na tajiri wake au atoe namba za simu za wafanyabiashara wengine wa ng'ombe ambao waliuza nao jambo ambalo alishindwa kutekeleza na hatimaye wakampiga kichwani kwa kitu kizito kilichosababisha afariki dunia.
Alisema Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kukagua tukio hilo muda mfupi baadae lakini hadi sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo ambalo linaonesha kulikuwa kuna kufahamiana baina ya waharifu na watu waliouawa.
No comments:
Post a Comment