Pages

KAPIPI TV

Thursday, December 25, 2014

MAJAMBAZI WAWILI WATEKWA MMOJA AAMUA KUJITOSA ZIWANI-KIGOMA

Baadhi ya Wavuvi Ziwa Tanganyika
 Na Magreth Magosso, Kigoma

Majambazi  wawili kutoka nchini jirani ya kidemocrasia ya Congo DRC wametekwa na kupigwa  na  mmoja kujitosa ziwani baada ya wavuvi wapatao 13 wanaofanya shughuli za uvuvi  katika Ziwa Tanganyika mwalo wa Muyobozi Jimbo la Kigoma Kaskazini  Mkoa wa Kigoma,kwa kuchoshwa na kitendo cha kuporwa zana za uvuvi kila wakati ziwani humo .

Awali  Saa 7.usiku majambazi hayo yakiwa  na silaha aina ya panga na bunduki za bandia katika mtumbwi wa kusoza walifika katika mwalo wa Muyowozi na kufanikiwa kumteka mvuvi mmoja aliyejulikana kwa jina la Seleman Ismaili na kumwamuru aendeshe mtumbwi mkubwa wenye injini kwa ajili ya kubeba injini wanazoendelea kuiba  usiku wa Desemba,23 kuamkia 24 mwaka huu

Akizungumza kwa niaba ya wavuvi, Selemani Ismaili alisema Desemba 23, 2014  baada ya kuiba mashine mbili katika mwalo wa muyowosi walishinda majini kwa masaa 24 hadi Desemba 24 mwaka huu usiku wa saa  7 walingia katika mwalo wa kagongo na kuiba mashine tatu na lita 44 za mafuta .

Alisema baada ya kuiba hizo mashine tatu aliwaelekeza wavuvi walioporwa mashine hizo kuwa majmbazi hayo hawakuwa na silaha zaidi ya panga na bunduki hewa waungane wawapige ,kitendo cha kuwapa ishara wavuvi 12 walioporwa ,ghafla walianza kupambana
 na majambazi  na mmoja alijitupa ziwani.

Ismaili alisema walimchangia  jambazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kifo  na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake hasa maeneo ya usoni na mkononi,Kwa upande wa Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Maweni  Dkt.Fadhili Kibaya alipoulizwa juu ya hilo alisema ni kweli walipokea majeruhi  kutoka kwa askari polisi  majira ya saa 10.00 alfajiri .

Dkt.Kibaya alisema majeruhi huyo anaendelea vizuri na anaongea kwa tabu kutokana  na majeraha sehemu za mdomoni na usoni na mikononi huku   Mwenyekiti wa wavuvi Sendwe Ibrahim alisema alipokea taarifa kutoka kwa wavuvi juu ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa mashine 4 lakini kwa juhudi husika wamedhibiti wahalifu  na mashine zipo kituo cha polisi cha kati .
 
Baadhi ya wamiliki walioibiwa mashine hizo Masabo Kaluhiga na Magombo Hassan kwa nyakatio tofauti walisema awali walikuwa na mashine 7 lakini kwa sasa wamebakiwa na mashine mojamoja ambazo nazo ndo hizo zilizonusurika kuporwa .

Kwa upande wa Ubalozi mdogo wa DRC-Congo Ricky Molema alisema sheria ichukue mkondo wake  na aliyelazwa hopsitali ya rufaa maweni akipona aadhibiwe kwa mujibu wa sheria ya Tanzania ,na  kwamba  hana ushirikiano na wahalifu.

Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma   Jafari Mohamed alisema ni  kitendo cha kishujaa kwa kijana Seleman Ismaili na hivyo  amempa motisha na atakuwa miongoni mwa  kundi la askari polisi waliofanya kazi kwa weledi kwa mwaka 2014 na atapata motisha na cheti cha kusaidia kulinda mali za raia .

No comments: