Baadhi ya maeneo yaliyoathiliwa na uharibifu wa mazingira kutokana na wingi wa Mifugo Katika Halamshauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda.(Picha na Kibada Kibada Katavi_) |
Na Kibada
Kibada –Katavi
Makala
Sekta ya
Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inakabiliwa na Changamoto
mbalimbali hali inayofanya sekta hiyo
kutafuta mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo uharibifu
mkubwa wa mazingira kutokana na wingi wa mifugo uliopo kuliko ukubwa wa eneo la
kufugia mifugo hiyo.
Baadhi ya
Changamoto hizo ni kuwepo idadi kubwa ya mifugo katika halmashauri,Uzalishaji
mdogo wa mazao ya mifugo kama nyama na maziwa na kipato kinachotokana na uwepo
wa mifugo hiyo katika Halamshauri.
Changamoto
nyingine ni upatikanaji mdogo wa mbegu
bora za mifugo hususani ng’ombe,eneo dogo la malisho ukilinganisha na Idadi
ya mifugo iliyopo kwenye Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda.
Pamoja na
kuwepo kwa wingi wa mifugo pia magonjwa
mengi ya mifugo kama ndorobo,ndigana kati na homa ya mapafu nayo ni moja ya
changamoto inayoikabili sekta ya mifugo Katika Halmashauri ya Mpanda.
Halmashauri
ya Mpanda ambayo ni moja ya Halmashauri katika Mkoa wa Katavi ina idadi ya Ng’ombe
wapatao 87,928,mbuzi 44,348,Kondoo 8,712,Nguruwe 2,237, mbwa 7425,na kuku
141.832 hata hivyo uwepo wa mifugo hiyo
bado haijatumiwa vizuri na kubadili
maisha ya wakazi wa Halmashauri hiyo na mkoa kwa ujumla kiuchumi na kuinua pato
lao kiuchumi.
Tafiti
zinaonesha iwapoidadi ya mifugo hiyo iliyopo ikitumiwa vizuri inaweza kuleta
tija na kuwaondolea umasikini wananchi katika maeneo husika.
Kwa mantiki
hiyo wataalam wa sekta ya mifugo wanayo kazi kubwa mbele yao kuhakikisha
wanatumia elimu yao kuwabadili wafugaji waweze kufuga ufugaji wenye tija
tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo ufugaji umekuwa wa kutokuwa na tija na kila
kukicha imekuwa ni mivutano na migogoro kati ya wakulima na wafugaji ingawa
hali hiyo bado haijatokea katika Halmashauri ya Mpanda lakini tunashuhudia maeneo
mengi hapa nchini hususani Mkoani Morogoro,wilaya ya Kilosa na Kilombero,Mkoani
Pwani ,na Arusha na Tanga wakulima na wafugaji migogoro ya kila mara.
Uwepo wa
mifugo mingi katika Halamshauri ya wilaya ya Mpanda pia kumeambatana
nanUharibifu wa mazingira kutokana na wafugajinhao kuhamahama na wengine kutumia njia hiyo kwa kufyeka miti
na mistu kwa shughuli za kilimo kwa kuwa wafugaji walioko katika Halmsahauri ya
Mpanda hao hao ndio wakulima.
Uchunguzi
uliofanyika kwa baadhi ya maeneo Mbalimbali Wilayani Mpanda inaonesha maeneo
mengi yanaoonekena kuathiri na Uharibifu wa mazingira na iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kwa haraka maeneo
hayo yanaweza kugeka jangwa.
Baadhi ya maeneo
yaliyoathirwa na uharibifu wa mazingira kutokana na mifugo ni bonde la Mto Katuma ambao ni tegemeo kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi hususani Mbuga
ya Katavi ya Katavi ambayo wanyama walioko huko hutegemea kupata maji kutoka
bonde la mto huo ambalo hutiririsha maji yake kupitia vijito vyake kupeleka
hifadhi ya Katavi.
Mbali ya
kutegemewa kwa ajili ya maji ya wanyama kama viboko na wengineo pia bonde la
mto huo wa Katavi ndilo linalotegemewa kwa kilimo cha mbuga unaozalishwa kwa
wingi katika maeneo ya Bonde hilo na kuwasaidia kuwaingizia pato wananchi
Mkoani humo.
Kwa wastani
uharibifu ni mkubwa sana kwa maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda kwa Kata za Kabungu,Mishamo, Mwese,Karema Mpandandogo Sibwesa, Kasekese
kote maeneo hayo yamejaa mifugo na uharibifu wa mazingira ni mkubwa mno
ukilingansha na hali iliyopo ya mifugo.
Akizungumzia
hali ya uharibifu na kuoneshwa alivyoguswa na hali hiyo na kuamua kuchukua
hatua za makusudi kuhakikisha uharibifu huo unafanyiwa kazi kwa kutoa elimu
zaidi kwa wananchi waelewe umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kuwa na mifugo
michache inayoweza kuwa na tija.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah anasema hali ya
uharibifu wa Mazingira ni mkubwa mno katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri
hiyo,kila eneo miti inakatwa hovyo bila kujari na hatua zisipochukuliwa ipo
hatari ya kutoweka kwa misitu hiyo ambayo inaonekana kuwa ni mingi lakini
ukweli ni ndio huo kutabaki kweupe wakati miti ilikuwepo kilaa kota ya Wilayah
ii.
Kwa kuliona
hili Mkurugenzi huyo amesema Halmashauri imeamua kuchukua hatua za kuweka
mikakati kwa kushirikiana na Idara ya
Maliasili kuanza kuelimsha jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na kuwapa
elimu wafugaji wafuge ufugaji wenye tija.
Mbali ya mikakati hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na wahisani
wa Tuungane na Taasisi ya Utafiti wa
wanyama aina ya Sokwe yenye Makao yake
Mkoani Kigoma Janegoodle (JGI)
wameanza mkakati wa kuimarisha kuvijengea
uwezo vijiji ili viweze kulinda
misitu kwa kutumia mpango wa matumizi
bora ya ardhi, pamoja n ulinzi wa mistu inayosimamiwa na vijiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Estomihn Chang’ah anaeleza kuwa katika Mpango huo Halmashauri imeanza kutoa
mafunzo kwa kuwapeleka Vijana wanne
wanne kwa kila kijiji wamepelekwa kupata mafunzo walikwenda kuhudhuria mafunzo
hayo katika chuo cha Hifadhi ya wanyama pori cha Pansiasi Mkoani Mwanza kwa kipindi
cha miaka mitatu.
Chang’ah anaeleza kuwa vijana waliopata mafunzo wanatoka
katika Vijiji vya Lwega, Mwese,Mpembe,Katuma,Vikonge,Isenga Bulamata na Bugwe
na jumla yao wapo( 17) walianza mafunzo hayo kuanzia Augosti 16,mwaka 2011 na
kuhitimu Novemba 15,mwaka 2014.
Kwa ajili ya kuwajengea uwezo waweze waweze kusaidia kulinda mistu na ardhi inayoharibiwa
katika halmashauri hiyo na mistu kama haikulindwa iko hatarini kutoweka na
kubaki jangwa.
Akizungumzia lengo kuu la kuunda kikosi cha watu 20 katika
kila kijiji ambacho kitaitwa ulinzi wa mistu yaani( Forest Gurd) ambacho
kitasaidia kulinda mazingira na mistu katika vijiji.
Wakiwa chuoni huko walijifunza kozi za aina mbalimbali
zitakazosaidia katika suala la uhifadhi wa mistu na kulinda mazingira, baadhi
ya kozi walizosoma ni matumizi ya silaha,sheria ya uhifadhi wa wanyama hima
sheria,uhifadhi wa mistu na matumizi endelevu ya ardhi.
Kozi nyingine ni usomaji wa ramani,huduma ya kwanza, Ikolojia
na usimamizi wa ardhi na rasilimali za mistu,Hifadhi za wanyamapori,Elimu ya
uhifadhi kwa jamii,na Elimu ya Sayansi ya
kuwajengea jami mahusiano, elimu ambayo itasaidia katika uhifadhi wa
mistu katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Akasema mafunzo yatakayofuata yataambatana na semina za
kawaida kwa hao vijana na viongozi wa vijiji ili wafahamu umuhimu wa mistu, na
mafunzo hayo kwa vijana yatakua endelevu lengo ikiwa ni kufanikia vijiji 15
katika Halamshauri ili waweze kulinda mistu ambayo imeharibiwa vibaya na
wavamizi wa mistu.
Uanzishwaji
wa kikosi cha ulinzi wa mistu ya Halmashauri cha ulinzi wa misitu ya kijiji
kitasaidia kusimamia ukataji wa mistu na
uharibifu wa mazingira katika maeneo ya hifadhi za mistu ya vijiji ili waweze
kuilinda wananchi wenyewe kwa kuelimishwa na askari wa kikosi cha ulinzi wa
mistu wanaotoka katika maeneo ya vijiji ambao wamepatiwa mafunzo na Halmashauri
kwenye chuo cha wanyapori Mkoani Mwanza
Kwa upande
wake Kaimu Afisa Ardhi, na Maliasli Halamshauri ya Wilaya ya Mpanda Lucas
Nyambala anaeleza kuwa pamoja na kuweka mkiakati hiyo ambayo imeanza
kutekelezwa kwenye vijiji pia Idara ya ardhi inatoa elimu kwa vijiji juu ya
matumizi bora ya ardhi na kupima vijiji ili kila kijiji kiwe na maeneo yake
ambapo wataweza kutekeleza mipango yao ya maenedeleo kweye ardhi iliyopimwa kwa
kuainisha matumizi ya ardhi yao kwa kuwa itakuwa inaonesha kila eneo shughuli
yake maalum tofauti na zamani hapo hata
migogoro ya aerdhi na uharibifu wa mazingira utapungua kama siyo kwisha kabisa.
Kwa kutumia
mpango wa matumizi bora ya ardhi kila mtu ataheshimu makubaliano hayo kwa kuwa ardhi ya kijiji
itakuwa inafahamika matumizi yake hivyo
hakuna mtu atakayeumia ardhi tofauti na makubaliano yaliyowekwa na kijiji,hata
miji nayo itaonesha wapi huduma za jamii ziwekwe ,makazi,eneo la ufugaji
,kilimo na huduma nyingine zote zitakuwazimeainishwa kwenye ramani ya ardhi ya
eneo husika la kijiji.
Nyambala
alieleza kuwa Kwa kuanzia mpango wa matumizi bora ya ardhi na upimaji wa maeneo
ya vijiji zoezi limefanyika la matumizi
bora ya ardhi na kupima maeneo ya ardhi katika vijiji vya Vikonge,Majalila, Mpandandogo.mwese,Mpembe
na kutolewa hati miliki za kimila baada ya kupimwa viwanja katika kijiji cha Vikonge ambapo zoezi hilo
linaendelea maendeo mengine ya Kata ya Mpandandogo,Karema,Sibwesa kazi hiyo
inafaa kuigwa na maeneo mengine ili kuepusha uharibifu wa mazingira.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima katika suala la uharibifu wa
mazingira na ufugaji wenye Tija amekuwa akilipigia keleke kila siku
akaenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa anashanga kumwona mfugaji anafuga
hovyo huku watalaama waliosomeshwa na serikali wapo wanashindwa kuwa
saidia wananchi kuepukana na umasikni akasisitiza watumie taaluma
kuwasaidia wananchi wao hapo ndipo watakapokuwa wametumia vizuri taalama
yao.
No comments:
Post a Comment