Na Kibada Kibada-Katavi
Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Paza Mwamlima amezindua Mtambo wa Kuzalisha Kimiminika cha
Nitrogeni utakaotumika katika kuhifadhi
mbegu bora za mifugo kwa ajili ya
uhamilishaji mifugo na kuwezesha upatikanaji wa
kosaafu za ng’ombe zenye tija.
Akitoa Taarifa ya Mtambo huo, kwa Mkuu wa Wilaya Afisa Mifugo kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi Laurensi Elias ameeleza kuwa Mtambo huo uliletwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi tangu mwezi juni mwaka huu na usimikwaji wake umekamilika mwezi septemba mwaka huu shughuli iliyofanywa na Kampuni ya Cooporation Group Ltd
Amesema gharama za Mtambo huu hadi kufukishwa Wilayani Mpanda umetumia kiasi cha shilingi milioni 400 pamoja na gharama za usimikaji zilizogharimu kiasi cha shilingi milioni 37.2 hivyo kufanya jumla yote kuwa shilingi milioni 437.290,950/-
Mtambo
huo ni aina ya Cryomech 120 una uwezo wa kuzalisha lita 5 kwa saa,
kiasi hiki huzalishwa baada ya muda wa kuwa tayari takribani saa nne
baada ya mtambo kuwashwa.
Ili mtambo uweze kuanza kazi kinahitajika kiasi cha shilingi milioni 39.7 kwa ajili ya kununulia vifaa na gharama ya kuwapeleka watalaam kwenye mafunzo ili waweze kusaidia kuendesha mtambo huo.
Amefafanua kuwa Ili mtambo ufanye vizuri ni lazima mambo ya umeme sahihi na wa kutosha uwepo, mfumo sahihi wa maji ya kutosha kwa ajili ya kupooza mtambo wakati wa uzalishaji,uwepo wa mzuunguko mzuri wa hewa ya kutosha isiyo na joto pamoja na usafiwa kutosha kuzuia vumbi inayoweza kuathiri mtambo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah ameeleza kuwa mtambo huo ni wa kisasa na hapa nchini ni unapatikana katika Mkoa wa Arusha,Iringa na Mbeya Pekee na huu ulioletwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda utasaidia sana kuhudumia,Mikoa ya Kigoma,Rukwa Tabora,Mbeya na Iringa nao watanufaika na mtambo huo kwa kuboresha mifugo kwa njia ya uhamilishaji.
Aidha utaongeza kipato cha Halmashauri kwa njia ya kuuza kimiminika katika taasisi mbalimbali kama Hospitali na maeneo mengine ya jirani na mapato yatokanayo na gharama za uzalishaji,Pia utainua kipato cha Taifa na wafugaji kwa kuuza ng’ombe waliobora na wenye tija kuboresha lishe ya mwananchi.
Pia itapunguza maambukizi ya magonjwa ya mifugo yanayotokana na kupandisha ng’ombe kwa kutumia madume mfano ugonjwa wa kutupa mimba.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameshauri Halmashauri kujenga urafiki na wafugaji kwa kuwapa elimu ili wawe pamoja wafugaji wote na utoaji wa huduma kwa kutumia mitambo huo utakuwa natija tofauti na sasa wafugaji wakiwaona watalaam wanawakimbia wanakuwa kama maadui.
Elimu itolewa kwa wafugaji waone mtambo huo kuwa utawasaidia kubadili hali ya ufugaji wao.
No comments:
Post a Comment