Pages

KAPIPI TV

Saturday, December 6, 2014

LIPUMBA AMTAKA RAIS KIKWETE KUTEKELEZA MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU ESCROW,MAANDAMANO MAKUBWA YANUKIA KUPINGA UFISADI

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Prof.Ibrahimu Lipumba akizungumza na wakazi wa wilaya ya Sikonge wakati wa ziara yake ya siku saba mkoani Tabora ambapo alitumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na changamoto za umasikini wa wananchi pamoja na kuzungumzia Sakata la Escrow huku akimtaka Rais Kikwete kutekeleza maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu  kuwawajibisha baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge na mawaziri wanaodaiwa kuchota mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Tageta Esrow ambazo ni pesa za walipakodi na wananchi wa Tanzania.Prof.Lipumba alisema endapo Rais Kikwete ataacha kutekeleza maazimio hayo ya Wabunge,wao kama UKAWA wanakusudia kuitisha maandamano makubwa nchi nzima kupiga UFISADI uliofanywa na viongozi hao.
Naibu Katibu mkuu Tanzania bara na mbunge wa vitimaalum CUF Bi.Madgalena Sakaya akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea namna ambavyo Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi inavyoshindwa kutekeleza Sera zake na kusababisha umasikini endelevu kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza katika mkutano huo wa hadhara
Naibu mkurugenzi wa habari na mawasiliano kwa umma CUF Bw.Abdul Kambaya akizungumza katika mkutano wa hadhara ambapo aliwataka wananchi kukubali mabadiliko kwa kuviunga mkono vyama vya upinzani wakati wa chaguzi mbalimbali za viongozi zinapojitokeza ili kuhakikisha wanaondoa viongozi wasiofaa ambao wapo kwenye chama cha Mapinduzi.
Mmoja kati ya Wabunge wa visiwani Zanzibar Bw.Rashid Ali Abdallah akizungumza katika mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Kojan Zanzibar kwa tiketi ya CUF Bw.Rashid Ali Omari
Baadhi ya wananchi wakiwa wametulia na kusikiliza mkutano huo.

Prof.Lipumba akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya ya Sikonge mara baada ya mkutano wa hadhara katika viwanja vya TASAF Sikonge.






No comments: