Pages

KAPIPI TV

Friday, December 19, 2014

FEDHA ZAPORWA ENEO LA MSIKITINI ZANZIBAR,NI EURO 1000 NA SHILINGI MILIONI TANO ZA KITANZANIA

Umati mkubwa wa wananchi wakistaajabu tukio hilo la wizi wa fedha eneo la msikitini.


 Na Haroub Hamisi -Zanzibar
Watu wasiofahamika wamevunja kioo cha gari na kuiba pesa Euro 1000 na shilingi milioni tano za kitanzania.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka eneo la tukio mwenye gari  hilo aina ya Landcruiser  lenye nambari za usajili Z 977 BM alifika na kuliegesha na kisha kuingia Msikitini kusali sala ya Ijumaa katika Msikiti wa eneo la Mlandege mjini Zanzibar.

Aidha baada ya kuegeshwa gari hilo lilitokea gari jingine nyuma yake ambalo mtu mmoja alishuka akiwa na Panga mkononi na kuanza kugonga kioo cha gari hiyo na kufanikiwa kufungua mlango na kutoa mkoba uliokuwa umehifadhiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha na kutoweka nacho kusikojulikana.

Hata hivyo imeelezwa kuwa askari wa Jeshi la polisi walifika eneo la tukio kwa lengo la kufuatilia sakata hilo la uporaji.





No comments: