Pages

KAPIPI TV

Thursday, November 6, 2014

VYAMA SITA VISIVYOKUWA NA WABUNGE VYAAMUA KUSHIRIKIANA KATIKA CHAGUZI ZIJAZO

1Mwenyekiti wa Chama cha UPDP na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba Mh. Fahmi Dovutwa akitoa taarifa ya ushirikiano wa Vyama sita vya siasa visivyokuwa na wambunge katika uchaguzi wa Serkali za Mitaa, Wabunge na Rais unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu mpaka mwaka 2015 ambapo uchaguzi wa Wabunge na Rais utafanyika.
“Dovutwa amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo vyama vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini  hakuna sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana tu ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama vilivyokubaliana kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA, UMD, UMD, UPDP NA AFP ,  Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
5
Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Yusuf Manyanga  akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.
3
Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Yusuf Manyanga , Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini

No comments: