MWANAMKE
mmoja mkazi wa Sigunga
Kitongoji cha Kawibiri Wilaya ya Uvinza,
Mkoani Kigoma Jasmin Kassim amelazimika kufanyiwa upasuaji wa kuunga mifupa ya mikono yote miwili katika Hospitali ya misheni ya Heri iliyopo wilayani kasulu ,baada
ya kujeruhiwa vibaya kwa
upanga na mumewe kufuatia madai ya kukaidi kutoa
unyumba.
“Baada
ya kumkatalia alitoka nje na alirudi
akiwa ameshika upanga ghafla akaanza kunipiga
na kisha kunikata mikono
yote miwili kuja kuzinduka nikajikuta nipo zahanati ya kijijini,nikashonwa nyuzi zaidi ya tano ” alisema Jasmin.
Octoba
,30,mwaka huu mwanamke huyo Jasmini alihamishiwa katika
hospitali ya Rufaa ya Maweni iliyopo Manispaa ya kigoma Ujiji ambapo alilazwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina ikagundulika mifupa ya mikono
imeachana na hivyo kushonwa kwa mara ya pili ili kusaidia mifupa kurudi
kwenye hali yake.
“Nashukuru
leo naongea shida bado ipo katika mifupa
,ndio haijaungana hivyo nasubiria nikiwa sijui ni lini mikono yangu itarudi
kama zamani” aliongeza Jasmin.
Nae
Muuguzi wa Zamu wa Wodi ya Kina mama Upande wa Majeraha na Wajawazito ,Yovita
Lushemeze , alisema kuwa Jasmin alipofikishwa hospitali hapo hali yake ilikuwa
mbaya kwani alikuwa na majeraha mikono yote miwili baada ya kukatwa mapanga.
“mifupa
ilifikiwa na panga na kukatika ila
mikono haikukatika moja kwa moja na madonda yalishughulikiwa na yanapona, bado
mfupa haijaunga inashughulikiwa” alisema
Lushemeze.
Alisema
jana aliruhusiwa akafanyiwe taratibu za matibabu zaidi wa upasuaji na wataalamu waliopo
katika hospitali ya Heri Misheni ,ambao wao watasaidia kuunga mishipa iliyojeruhiwa vibaya.
Ukosefu wa mawasialiano na boti la kisasa inachangia wahanga wa matukio ya ukatili wa
kijinsia kushindwa kusaidiwa kwa haraka,ambapo Mkuu wa dawati la jinsia la
Polisi Amina Kihando akiri tangu huduma
zianze rasmi 2007 hawajafika kwa wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika .
Hivyo,inachangia
washindwe kupata takwimu sahihi za matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani na kusihi wadau wa masuala hayo TAMWA,TGNP,TAWLA
na wengineo waweke mawakala washirikiane kubaini matukio ya aina
hiyo kwa lengo la kupunguza vitendo viovu.
No comments:
Post a Comment