Bibi mwenye umri wa miaka 60 akatwa sehemu zake za siri na mumewe ili akauze milioni tano,bibi huyo ambaye jina lake linahifadhiwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete anadaiwa kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala huko nyumbani kwao mtaa wa Kazaroho kata ya Mbugani manispaa ya Tabora....."Mume wangu alikuwa amekwenda kutembea akarejea nyumbani na mtu mmoja ambaye ni mganga wa tiba za asili ambaye alifika nyumbani hapo akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke,mimi nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala akanikata huku akiniamuru nisipige kelele"alisema bibi huyo akiwa kitandani hospitali kufuatia unyama aliofanyiwa na mumewe Bw.Mashaka Maziku.
www.kapipijhabari.com
www.kapipijhabari.com
No comments:
Post a Comment