Makamu
wa Rais akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Ruketngwe
kushoto kwa makamu wa Rais na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi
Stella Manynya wakimwongoza kuelekea Banda la Mkoa wa Katavi kupata
maelezo juu ya fursa za uwekezaji na maeneo ya uwekezaji katika mkoa
huu na kukagua bidhaa za wajasiliamali katika kongamano la uwekezaji
nalililoandamana na maonesho ya biashara ya SIDO yaliyofanyika mjini
sumbawanga kwenye viwanja vya Nelson Mandelea Mkoa Rukwa.
Dkt
Bilal akiwapungia mkono wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliofika uwanjani
kumpokea alipowasiri kufungua kongamano la uwekezaji Mjini Sumbawanga
kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tangantika.akiongozwa na mwenyeji wake
Mhandisi Stella Manyanya mkuu wa Mkoa wa Rukwa na mwenye Tsheti ya bluu
bahari ni Dkt Mary Nagu waziri wa uwezeshaji na uwekezaji.
Hapo Dkt Bilal Makamu wa Rais
akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo
alipowasiri kufungua kongamano la uwekezaji,
(Picha zote na Kibada Kibada -Rukwa)
………………………………………………………………………………………………….
Na Kibada Kibada –Rukwa
Makamu wa Rais Dkt Ghalib
Mohamed Bilal amewataka wale wote walio katika ngazi za madaraka
Serikali na kwenye mamlaka mbalimbali za maamuzi kuacha urasimu katika
kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanapoonesha nia ya kuja kuwekeza
katika Tanzania.
Dkt Bilal alitoa agizo hilo
wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mikoa ya Rukwa Katavi na
Kigoma liliofanyika Mjini Sumbawanga kwenye uwanja wa Nelson Mandela
Mkoani Rukwa.
Amesema watu wamekuwa na
mitazamo hasi katika sekta ya uwekezaji na vitega uchumi,akasema katika
uchumi wa leo bila uwekezaji hakuna maendeleo,uwekezaji utasaidia katika
kukuza uchumi,utasaidiakupunguza umasikini,kuongeza ajira katika nchi.
Dkt Bilal akaeleza kuwa uchumi
katika dunia ya leo ni uwekezaji kwa kuwa hata nchi ya China ambayo
uchumi wake ni wa pili kwa ukuaji duniani bado inakaribisha
wawekezajij,sasa itakuwa jambo la ajambo kwa nchi kama Tanzania
kuwakataa wawekezaji kuja kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta
mbalimbali.
Dkt Bilal akawahimiza wananchi
wenye uwezo kujitokeza kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo katika
ukanda wa Mikoa hii ya Ziwa Tanganyika.
Akazihimiza halamashauri kutenga
maeneo ya uwekezaji na kufungua milango ya uwekezaji kwa kuondoa
urasimu usiokuwa wa lazima watoe ushirikiano wa karibu kwa wawekezaji
wanapojitokeza kuwekeza katika mkoa mikoa hiyo.
Kila mmoja kwa nafasi yake atoe
ushirikiano wa karibu kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kwa kuwa
ana mchango mkubwa wa uwekezaji katika ukanda huu.
Awali Waziri wa Uwezeshaji na
uwekezaji Dkt Mary Nagu kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua
kongamano hilo alieleza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya
uwezeshaji kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji katika ukanda huu wa ziwa
Tanganyika
Akizungumzia fursa zilizopo za
uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika amewahimiza watu wajitokeza
kuwekeza katika ukanda wa mikoa hiyo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji ni
rafiki kwa kuwa sasa ukanda huu unafikika kwa urahisi kwa kutumia usafi
wa anga na barabara kwa kuwa miundo mbinu ya barabra imefunguka.
Kwa hiyo kazi iliyopo ni
kuimarisha uchumi wa nchi na hasa ukanda huu wa ziwa Tanganyika ambao
unafursa nyingi katika uwekezaji, akaeleza kuwa uendeshaji wa
makongamano ni utaratibu uliowekwa na serikali kwa ajili ya kuwezesha
makongamano kwenye kanda ambapo hadi sasa kikanda makongamano haya
yamefanyika katika kanda za Kaskazini, Mashariki, ukanda wa Ziwa,Kusini
na Kanda ya ziwa Tanganyika ambapo kote kuliko fanyika makongamano hayo
kumeonesha mabadiliko makubwa ya kukua kwa uchumi.
Akasema nchi ya Tanzania
inaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa na wawekezaji kuliko
nchi nyingine za Afrika Mashariki,ambapo katika kipindi cha mwaka jana
uwekezaji uliingia kiasi cha dola 1.87 milioni kwa mwaka jana,hata hivyo
uwekezaji huo unaelekezwa katika miji ya Mwanza, Dar es Salaam, Arusha
Pwani na Mbeya.
Awali wakuu wa Mikoa ya Rukwa
Mhandisi Stela Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe,na
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Salehe Machibya
walielezea fursa zilizopo katika mikoa ya kuweza kuwekeza katika maeneo
ya mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika ambapo fursa zipo nyingi.
No comments:
Post a Comment