Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 21, 2014

WAFUGAJI KAKONKO WAUA WATU WAWILI FAMILIA MOJA KISA KISASI...KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

WAFUGAJI   wanaoishi kijiji cha Minyinya Kata ya Nyamtukuza wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma,wamewashambulia  Baba  na mtoto  kisha kuwachoma moto hadi kufa kwa madai ya kuwaamuru  waoneshe walipo majambazi walioua  Mfugaji wa ng'ombe katika tukio la Octoba ,15,2014.

Akielezea  tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Minyinya Justini Kilegea   alisema tukio hilo ni  la kulipiza kisasi kwa wakulima ambapo wafugaji walihisi waliovamia na kuua mwenzao wiki iliyopita alitoka katika jamii ya wakulima hivyo walitaka waoneshe waliofanya tukio hilo jambo ambalo lilizua tafrani na kuanza kushambuliwa hatimaye kuwaua.

“sasa usiku wa Octoba ,19 kuamkia 20,mwaka huu ndipo wafugaji  walivamia nyumba za wakulima zipo hukohuko mashambani na kuzichoma moto na hatimae  kumuua mtu na mwanae Kachila Kahegele (48) na Lameck Kahegele (26) .

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho Daniel Paulo ,Jonas Matwa na Silace Kahebela walidai mwenyekiti wa kijiji hicho ndio chanzo cha mauaji baina ya wafugaji wageni na wakulima ,ambapo hugawa ardhi kinyemela ,bila kushirikisha wananchi ,hatua ambayo imekuwa ni chanzo  na  chokochoko za mapigano baina ya pande hizo  mbili.
 
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto alisema wafugaji hao walifika hapo wakisaka madini na walipokosa walianzisha kilimo na ufugaji  wa ngombe ukashamiri na hatimaye wakanzisha kijiji hali iliyowavutia wakazi wa Minyinya kuhamia huko mashambani  na 15,Octoba,2014  miongoni mwa wakulima waliua mfugaji  mmoja.

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma  Jafari Mohamed alipoulizwa juu ya mauwaji hayo ,alisema yupo nje ya mkoa ,hivyo hajapewa taarifa ya tukio hilo na kusisitiza kuwa kila raia anawajibu wa kutii sheria bila shuruti hata kama alionewa akithibitika anawajibika katika vyombo vya dola.

No comments: