Na Magreth Magosso,Kigoma
MWENYEKITI wa chama cha (CHADEMA) Mkoa wa kigoma Ally Kisala ametoa siku 14 za uwajibikaji kwa Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ramadhan Maneno endapo hatawadhibiti wanachama wa chama cha
Alliance Transparency For Change(ACT) kwa kitendo cha utovu wa nidhamu ,madili,kwa mujibu wa katiba ya Nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana katika mkutano wa hadhara
uliofanyika eneo la Mwanga urusi uliokuwa ukiwataka wananchama wake waache
kulumbana hoja na wanachama wa ACT na
kudai chama hicho kuwa ni SACCOS ya mtu mmoja ambaye analengo la kudhofisha
vyama vya upinzani .
Chanzo cha kupewa siku 14 ni kutokana na sintofahamu dhidi ya mgogoro wa eneo la urusi ambapo awali kulikuwa na Bango
la Chadema lililokuwa na wanachama wapatao 20,hatimaye wote wamejiunga na ACT na hivyo bango linatumika na ACT .
Hali iliyochangia Mkuu wa wilaya hiyo Ramadhan Maneno
kuwapa amri wanachama wa ACT na Chadema
wasitishe huduma zao kutpitia bango hilo la Urusi hadi suala litakapopatiwa ufumbuzi na vyombo
vya dola.
“nitatumia nguvu ya watu ili kutimiza uwajibikaji kwa mkuu
wa wilaya itakuwaje walitumie wao na
ndio maana Jeshi la Polisi wametoa bendera ya ACT lakini maneno anawabeba
nitatumia nguvu ya umma ,damu itamwagika na wataokota maiti” alidai Kisala.
Katibu wa Chadema wilaya ya Kigoma Frank Lucas alisema kwa
miezi mitatu siasa ya kigoma imegubikwa na lugha chafu ambazo hazina mashiko katika jamii,ilihali wanakabiliwa na
adha mbalimbali na kuwaonya wasilumbane hoja na wananchama wa ACT kuanzia jana
na kuendelea.
Akijibia hilo Mwenyekiti wa ACT Kigoma Ibrahim Sendwe
alisema siasa za kumwaga damu ni kawaida ya chadema na kudai suala hilo lipo
mahakamani na Octoba ,27,2014 kesi itaanza kusikilizwa ,huku akionya Jeshi la Polisi
waache kuingilia hoja za wanasiasa na kudai kitendo cha kuondoa bendera ya ACT
ni kuidharau Mahakama.
Mbali na hilo uongozi wa chadema wametumia zaidi y ash.200,000
kwa kununua katoni za juisi,matunda na
sabuni za Gwanji na kuzigawa kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya maweni ,Huku Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Fadhili Kibaya akiwaongoza
katika wodi ya kina mama,watoto na kina baba ili kufanikisha ugawaji huo.
Mjumbe wa Uongozi wa Chadema kanda ya Kati Taifa Alphonce Mbasa alisema
wamejipanga kubadili mwelekeo wa siasa kwa kutoa huduma zitakazowafikia wananchi moja kwa moja hasa kusaidia makundi tete likiwemo
wagonjwa na yatima.
No comments:
Post a Comment