Na Magreth Magosso,Kigoma
SINTOFAHAMU ya elimu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo
unaochangiwa na ugumu wa maisha katika Mkoa
wa Kigoma,imepelekea baadhi ya wazazi kuwauza
watoto wenye miaka 13 hadi 14 ,kwa ujira
wa malipo sh.70,000 kwa Mwaka kwa Jamii
ya wafugaji waliovamia pori la hifadhi lililopo katika kata ya Kagerankanda Tarafa ya Katoto wilayani kasulu.
Akifafanua hilo kwenye kikao cha madiwani kilichofanyika hivi karibuni kasulu mjini , Diwani wa kata ya kasulu mjini
Izack Mkemwema alisema wameligundua hilo katika operesheni ya kutathimini
uhalisia wa jamii ya wafugaji ambao wameingia kinyemela katika mapori
mbalimbali wilayani humo hasa pori la kagerankanda.
“hali mbaya biashara
ya binadamu inaendlea katika jamii zetu ,wazazi wanauza watoto kwa ujira wa
shilingi 70,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya kuchunga ng`ombe ,ambapo kisheria
ni kosa biashara ya binadamu lakini ipo na inatendeka kwa wakazi wetu “
alibainisha Mkemwema.
Diwani wa kata ya kagerankanda Joel Simon alisema hali hiyo
inachangiwa na hali ngumu ya maisha katika familia husika sambamba na jamii
kushindwa kuwajibika,kujitambua na uthubutu wa kukabiliana na changamoto za
maisha sambamba na watoto hukubali kutumiwa vibaya baada ya kukaidi kusoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya kasulu William Luturi alisema ili kubaini wahanga hao halmashauri kupitia wataalamu na
watendaji wa eneo husika watafanya uhakiki
wa watoto waliouzwa katika kaya
za wafugaji wasio rasmi kwa maslai ya kuweka ulinzi na kulinda haki za watoto
husika na sheria itachukua mkondo wake .
Luturi alisema walezi
wameacha majukumu yao kwa familia zao hali inayochangia watoto kuacha masomo
katika shule walizokuwa wakisoma ,badala yake hujiingiza katika ajira zenye
ukiukwaji wa haki za watoto kwa mujibu sheria mbalimbali zinazobainisha kulinda haki na
ulinzi kwa watoto na kuwasihi jamii watoe tarifa katika idara husika ili
kustawisha taifa na wilaya husika.
Kwa upande wa Mratibu wa asasi ya kusaidia watoto waishio katika
mazingira magumu ( KIOO) ya hapa Edward Simon alibainisha kuwa,walezi wanashindwa kuwajibika
kwa familia zao kikamilifu hali inayochangia watoto kutumikishwa kazi ngumu na
ujira mdogo ambao unalisha kaya husika .
Mkuu wa Dawati la jinsia kigoma Amina Kihando akiri watoto ni wahanga wa ajira haramu ikiwemo ya kuuza
miili hali inayochangiwa na elimu duni
miongoni mwa jamii hasa kwa mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi inatokana na ukata unaochangia Dawati hilo , kushindwa
kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na athari zake na namna ya kupunguza vitendo
hivyo ili kuthibiti maadili mema.
No comments:
Post a Comment