Madiwani wa vyama vya upinzani Chadema na Nccr-mageuzi
wilaya ya kasulu Mkoa wa Kigoma,wamesusa
kufanya uchaguzi wa makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo,kwa madai ya ukiukwaji wa haki,kanuni
na taratibu husika za kufanya uchaguzi huo.
Hali hiyo imetokana na muda mdogo wa mandalizi ya kuandaa majina ya wagombea wao kuwa haukuwa huru na haki kutokana na
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Masalu Mayaya kutumiwa vibaya na chama
tawala,hali iliyosababisha wapewe barua ya kuchagua majina ya wagombea wao siku
mbili kabla ya kikao cha baraza la madiwani hao ambacho kilifanyika
1,Agosti,2014.
Charles Kahise mgombea kupitia chama cha Nccr-Mageuzi
alisema halmashauri inastawisha madiwani wa ccm na kuupuza hoja mbalimbali za
vyama vya upinzani,ambapo wangefanya uchaguzi huo kwa kuzingatia wajumbe wa
kikao hicho na kudai kukosekana kwa wabunge wao Agripina Buyogera na Moses
Machali ni pigo kwao.
Mwenyekiti wa chama cha Nccr-mageuzi Hitla Joseph na Katibu wa Chadema wilayani hapo Haruna
Kwasakwasa kwa nyakati tofauti walisema ,wajumbe halali hawapo ndio kitu kilichochangia kugomea uchaguzi huo
huku akiwanyoshea kidole watumishi wa halmashauri hiyo kuwa ni sehemu ya chama
tawala hasa wanasheria husika.
Wakijibu tuhuma hizo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Masalu Mayaya na mwenyekiti wa halmashauri
William Luturi walisema kikao hicho ni cha kufunga mwaka wa fedha,walitoa siku
mbili kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Eid Fitri ndio sababu ya kusema
wapeleke majina ndani ya siku mbili si kwa utashi wa ccm bali uhalisia wa
mambo.
Walisema,walichohofia ni baada ya mbunge machali kutoonekana
katika kikao hicho walihofu watashindwa na kusababisha ccm kupitia mwakilishi
wa kiti hicho Benjamin Chakukura kujipatia ushindi kiulaini,kupitia wajumbe 18
wa ccm na mjumbe mmoja chama cha CUF Esta Kisomye na kanuni inaruhusu kufanyika
kwa uchaguzi huo.
Awali kikao kilitakiwa kifanyike Julai,28,2014 uchaguzi wa
makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo na 28,julai,mwaka huu kikao cha
madiwani na kuwasihi madiwani wa vyama
vya upinzani wakubali uwajibikaji na si kugoma.Wakatihuohuo Mwenyekiti umoja wa
vijana ccm kasulu Mbelwa Abdallah alisema elimu ndogo kwenye elimu kubwa lazima
sumu itumike.
Mbelwa alisema amegundua katika kikao cha baraza hilo
madiwani wa chama tawala hawana ubunifu katika kujibu hoja mbalimbali dhidi ya
serikali,hali inayoifanya halmashauri kushindwa kufikia malengo
kiutendaji,ambapo imekuwa na hulka ya kuwaondoa wakurugenzi kila wakati ambapo
kwa sasa Mwayaya ni mkurugenzi wa sita,wote wakitolewa kwa kushindwa
kuwajibika.
No comments:
Post a Comment