Na Magreth
Magosso,Kigoma
WANAFUNZI wa
Shule ya Msingi Airport iliyopo wilaya ya Kigoma Manispaa ya Kigoma
Ujiji, wanadaiwa kutumia mifuko ya Rambo kujisaidia haja zao ,baada ya kukosa choo zaidi ya miaka miwili,
ili hali uongozi
husika wanalifumbia macho changamoto hiyo.
Pia shule hiyo
inakabiliwa na adha ya ukosefu wa maji
sambamba na madawati 600 ,ili kukidhi hitaji la wanafunzi wapatao 1408 pamoja
na vyumba vya madarasa ,ambapo kila
darasa lina wanafunzi 173, hali
inayochangia uelewa finyu kwa wanafunzi husika.
Jamboleo
lilipiga hodi katika shule hiyo,baada ya kubaini Diwani wa kata ya Mwanga mjini
Moses Bilantanye Kuahidi kupeleka Mifuko ya Rambo shuleni hapo,ili kuokoa jahazi
la vifo kwa wahanga hao kutokana na choo chao kutitia.
“ shule ilitaka kufungwa kitambo
lakini wamezibaziba tundu mbili tu tena kwa shida ,wanafunzi hutumia sasa mimi
napeleka mifuko wiki ijayo ,ili
wajisaidie humo,” alianisha Bilantanye.
Kwa upande
wa Mwalimu Mkuu Yustus Fundi alipohojiwa
mifuko ya Rambo kutumika kwa
wanafunzi hao ili kujisitiri na maumbile
ya mwili alisema ni kweli hali inayochangiwa na ubovu wa matundu saba ya choo
sambamba na ukosefu wa maji.
Alisema
aliyekuwa mkurugenzi wa awali Alfred Luanda na ofisa elimu Shomari Bane walifika
katika shule hiyo na kutaka ujenzi ufanyike ndani ya wiki moja kuokoa janga hilo, kabla ya utekelezaji walihamishwa mkoani hapo.
Mratibu elimu kata ya husika Edes Ibrahim na kaimu mwalimu mkuu
Deogratius Rulakuze kwa nyakati tofauti
walisema Novemba,23,2012 walipeleka barua kwa wakuu wa idara na hakuna jipya
zaidi ya kila mwanafunzi anajua njia ya kujisitiri kwa namna yake.
Walisema walijaribu kuomba msada kwa BayPort na mkuu wa uwanja wa ndege mkoani hapo lakini
jitihada za kuwapatia hitaji hilo hakuna zaidi ya ahadi ya maneno .
Aidha Mtandao huu umeshuhudia baadhi ya wanafunzi Matilda Zephine na Neema Samweli
wakinyata kwa tahadhari kuingia katika choo hicho ambacho wakati wowote kitazama
chini kutokana na shimo kubwa lililotoboa tundu za choo hicho.
Walipoulizwa
sababu ya kunyata wakati wa kuingia chooni walidai wanaogopa kutumbukiwa na
kukiri hali hiyo inashawishi baadhi kuwa watoro hasa wakishikwa na haja wakienda
nyumbani nadra kurudi darasani kuendelea na vipindi vingine.
Akijibia
hilo Mwenyekiti kamati ya uchumi afya na elimu manispaa hiyo Moshi Said alisema changamoto ya vyoo katika shule za manispaa
kigoma ujiji ni makubwa hivyo katika
kikao cha Octoba mwaka huu 2014
watatenga bajeti ya kujenga matundu ya vyoo 200 kwenye shule zote zenye changamoto hiyo .
No comments:
Post a Comment