Kamishina wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akikata utepe
kuashilia uzinduzi rasmi wa Filamu ya The Minister katika hafla
iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo
Kamishina wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akifurahia mara
baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Filamu ya The Minister
katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaa,. Filamu
hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Equity Link Enterpreses ya jijini Dar
es Salaam ambapo inaelezea namna viongozi wa umma wanavo ishi katika
muktadha wa maadili miongoni mwa jamii zao.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzaia Bibi Joyce Fissoo akimpongeza Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara
baada ya kuzindua rasmi Filamu ya “The Minister” Filamu hiyo
ilimetengenezwa na Kampuni ya Equity Link Enterpreses ya jijini Dar es
Salaam inaelezea namna viongozi wa umma ambavyo utumia nyadhifa zao bila
kuzingatia maadili.Katika ni Muongozaji Mkuu wa Filamu hiyo na
Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hii Bibi. Deborah
Nyakirang’ani.
Msaani wa Filamu mbaye ameigiza
kama Mhe. Waziri katika filamu hiyo Bw. Julius Busee (Mr.Kakula)
akifanya mahojihano na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Filamu ya “The Minister” ambapo yeye ndiyo muhusika mkuu.
Katikati Kamishina wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda
akiangalia ngoma mara baada ya kuzindua rasmi Filamu ya The Minister
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kulia ni Muongozaji Mkuu wa Filamu hiyo
na Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hii Bibi. Deborah
Nyakirang’ani.
Wa kwanza kutoka kulia Mkurugenzi
wa Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Leah Kihumbi akiwa na baadhi ya wadau wa Filamu
wakiangalia Filamu The Minsiter ilipoonyeshwa kwa mara ya kwanza wakati
wa hafla za uzinduzi wake hivi karibuni katika Ukumbi wa Century Cinemax
jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzaia Bibi Joyce Fissoo akiwa katika picha ya pamaoja na wasanii
walioigiza akatika Filamu ya The Minsiter mara baada ya uzinduzi
kukamilika, Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Equity Link
Enterpreses ya jijini Dar es Salaam ambapo inaelezea namna viongozi wa
umma wanavo ishi katika muktadha wa maadili miongoni mwa jamii zao.
Picha zote na Frank Shija
Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM
…………………………………………………………………………………
Na Frank Shija, WHVUM
Viongozi wa umma wametakiwa kuendeleza uzalendo ambao muasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alituachia.
Rai
hiyo himetolewa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda alipokuwa akizindua Filamu ya “The
Minister” mapema hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Jaji
Kaganda alisema kuwa viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha uzalendo unakua hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufanya kazi
kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria badala
ya kuendelea kupiga kelele bila vitendo.
Aidha
Jaji Kaganda aliongeza kuwa watumishi wa umma wanaongozwa na kanuni za
maadi ya utendaji ambapo alitaja sheria ya maadili ya viongozi wa Umma
Na. 13 ya mwaka 1995 na kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma za mwaka
2005 ambapo alisema mtumishi akizingatia ni dhahiri kwamba atakuwa
mzalendo wa kweli.
Aliongeza
kuwa amefarijika kuona wasaniisasa wameamua kutumia vipaji vyao kutoa
Elimu ya maadili ambapo kupitia Filamu ya The Minister viongozi wengi
watajifunza ana kujisahihisha pale walipoteleza. Alisema Jaji Kaganda
Jaji
amesema kuwa maadili ni suala nyetu kwani bila maadili haki haipatikani
hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuhakikisha
kunajenga jamii yenye maadili.
Katika
hali ya kuonyesha amevutiwa na Filamu hiyo Jaji Kaganga ametangaza
rasmi kuwa Ofisi yake itatumia Filamu hiyo kama kielelezo rasmi wakati
wa utekelezaji wa shughuli za uelimishaji kwa umma.
”
Nimefurahishwa sana na maudhui ya Filamu hii naomba nipatiwe nakala
angalau tano hili nami niweze kuwa na vielezo vya kutumia pindi
tunapotekeleza majukumu yetu ya kuelemisha umma juu ya maadili ya
viongozi” Alisema Jaji Kaganda.
Kwa
upande wake Muongozaji wa Filamu hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Equity Link Enterprises Bibi. Debora Nyakirang’ani amesema kuwa wazo
hilo la Filamu ya The Minister baada ya kubaini kuwa wasanii wengi
ujikita zaidi katika kucheza filamu zenye mafundisho tofauti na kusahau
eneo nyeti la maadili.
Kushuka
kwa maadili miongoni mwa jamii imekuwa ni chachu ya vijana wengi
kutokuwa wazalendo wa nchini yao tena badala yake watu wamebaki kuwa
wabinafsi zaidi.Hivyo nimatarajia yangu kwamba kupitia Filamu hii wwatu
watabadilika na kurudu katika mstari ulionyooka. Alisema Bibi.
Nyakarang’ani.
Filamu
ya The Minister ni filamu ya kitanzania iliyoandaliwa na kutengenezwa
na Kampuni ya Equity Link Enterprises,katika Filamu hiyo inaelezea namna
mhusika mkuu alivyobadilika ghafla mara baada ya kupata wadhifa wa
Uwaziri, na jinsi ambavyo alikuwa akiishi katika maisha yake binafsi
yakionyesha azingatii maadili yake ya kazi ipasavyo
No comments:
Post a Comment