Pages

KAPIPI TV

Monday, August 25, 2014

MTOTO APOTEZA MAISHA BAADA YA KUGONGWA NA LORI LA MCHANGA KWA MAKUSUDI,DEREVA AKIMBIA.

Mwili wa mtoto Cecilia Cecilaus(10) ukishushwa katika makaburi ya Tanesco kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora ambapo mtoto huyo imedaiwa kuwa aliuawa baada ya kugongwa na Lori la mchanga pembezoni mwa barabara hatua ambayo kwa mujibu wa mchoro wa askari wa Usalama barabarani umeonesha kuwa dereva wa Lori hilo aina ya Fusso lenye nambari za usajili T 146 CWX alimgonga kwa makusudi baada ya kumfuata nje ya barabara ambapo vipimo vilionesha dereva wa Lori hilo alipita upande wa kulia umbali wa Futi 11 kati ya Futi 40.8 za upana wa barabara hiyo na kumgonga mtoto huyo ambaye alipoteza maisha baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete,Tukio hilo ambalo lilitia simanzi kwa watu walioshuhudia kitendo cha kinyama alichofanya dereva huyo ambaye alikimbia na Lori hilo huku akiwa amezima taa wakati mtoto huyo aliyekuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kiloleni akiachwa anagaagaa chini na kuvuja damu nyingi.
Mama mzazi wa mtoto Cecilia akishiriki mazishi ya mtoto wake katika makaburi ya Tanesco
Baadhi ya ndugu na jamaa watizama kwa huzuni kubwa kaburi la mtoto Cecilia baada ya kuzikwa.



No comments: