
Wawakilishi
wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati,
wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane
Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Vikundi
vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha
Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya
pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi
wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada
wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa
niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL)
imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam ikiwa ni
kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr.
Msaada huo wenye jumla ya thamani
ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL, Dar es Salaam
Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye
alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa kampuni yao kusaidia makundi na
taasisi na idara anuai kwa masuala ya kijamii.
Bi. Mwakalebela alivitaja vituo
ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima
cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na
Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya jijini Dar es Salaam.
“…Msaada huu ni maalum kwa ajili
ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo hili la leo ni utaratibu
wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na idara mbalimbali kuhusu
mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii,” alisema Bi. Mwakalebela
kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.
Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo
ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga, unga wa sembe,
maharage pamoja na katoni za juisi za maboksi.
Kwa upande wao wawakilishi wa
vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka
watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr
kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment