Na Magreth
Magosso,Kigoma
IMEFAHAMIKA
kuwa,Mabomu yenye uwezo wa kulipua Ndege za kivita angani yaliyotupwa ziwa
Tangayika Mkoa wa Kigoma,yanaendelea kuibukia ufukwe wa bandari kongwe ya
forodhani iliyopo manispaa ya kigoma
ujiji.
Akifafanua
hilo Kamanda wa Polisi mkoani hapa Frasser Kashai alisema Julai,27,mchana
walipata taarifa uwepo wa bomu kubwa linalotumika kutungua ndege angani maeneo
hayo ambapo watoto walikuwa wakicheza nalo.
Alielezea
kwamba,mabomu hayo yalitupwa katika ziwa hilo kwa miaka kadhaa ambapo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ,ziwa
linatema mabomu hayo hali inayohatarisha
usalama wa wananchi walio wengi hawajui bomu
hatimaye watoto huyatumia kama mpira.
“wenzetu wa
JWTZ kikosi 24 wamelichukua na kwenda kulifanyia kazi,wananchi watoe taarifa
mapema pindi waonapo bomu lolote katika fukwe ya forodhani ambayo ni sugu kwa
kutema zana hizo kwa usalama wa jamii “ alibainisha Kashai.
Mkazi wa kigoma Ujiji Hussein Kaliango alipohojiwa ni kweli awali
bandari ya forodhani ilitema bomu la
aina hiyo,alisema ni kweli matukio ya bomu hujitokeza ambapo mika mitatu
iliyopita mwananchi mmoja alikufa kwa bomu la aina hiyo.
Alisema
baada ya kuliokota akalitumia kama figa la jikoni ,mwisho wa siku moshi mkubwa
ulikuwa ukifuka sana yeye alijua ni kuni inatoa moshi ndipo alipoingia ndani ili akapulize ndipo umauti ukamkuta .
No comments:
Post a Comment