Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 17, 2014

WATANO WAPOTEZA MAISHA KIGOMA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

 
Na Magreth Magosso,Kigoma
WATU  watano  wamekufa katika matukio tofauti mkoani Kigoma,akiwemo Moshi Suleiman (45) amekufa kwa kutumbukia ziwa Tanganyika, baada ya kukumbwa na hali ya  ugonjwa wa kifafa.
 
Akifafanua hilo  Ofisini  kwake kigoma Ujiji Kamanda wa Polisi Mkoani hapa,Frasser Kashai alibainisha kuwa,Juni,14,2014 saa 1.00 jioni  eneo la Bangwe ziwani katika manispaa ya kigoma Ujiji  Suleiman akiwa anatembea pembezoni mwa mwalo huo ghafla alishikwa na kifafa kilichosababisha atumbukie majini,hivyo kunywa maji mengi na kusababisha umauti wake.
 
Katika tukio la pili   Juni,15,Mwaka huu eneo la kijiji cha Kizazi tarafa  ya Mabamba wilayani Kibondo, Mtu mmoja anayesaidikiwa raia  kutoka nchi  ya Burundi amekutwa amekufa  na mwili wake  kutelekezwa kandokando ya Barabara kubwa kijijini hapo.
 
“ wanakijiji wamehisi huenda ni raia wa huko kutokana na  kutokumfaham  kijijini hapo ,ni ngumu kupata tarifa zake muhimu aaah  marehemu  ni mwanaume ,uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa mauwaji hayo” alisema Kamanda huyo.
 
Wakati  huohuo  Juni,15,2014  Saa 6.00  usiku katika  kijiji cha kitanga Wilaya ya Kasulu eneo la Mulimi mashambani  Mkulima Mmoja Rhino Ntakobakiza ( 75) amekufa kwa ajali ya moto,baada ya nyumba waliyokuwa wamelala na mkewe Janeroza Ntakobakiza (55) kuungua moto .huku chanzo cha moto huo hakijulikani.
 
Katika tukio la mwisho  Juni, 14,2014 saa 1.05 jioni katika  kijiji cha Mugombe tarafa ya Buhoro wilayani kasulu ,Watu wawili Beda Alphonce(44) na  Jastine Jacob (01)  wamekufa papo hapo , Baada ya  basi walilopanda kupinduka na kusababisha kifo chao .
 
Kamanda Kashai alisema Basi la Kambas  aina ya Scania lenye namba za usajili T607 ARR linalofanya safari zake Kahama  Kigoma  mali ya Said Nassoro ambalo liliendeshwa na Issa Salum kugongana uso kwa uso na gari  aina ya Hiace iliyokuwa ikitoka kasulu kwenda kibondo likiendeshwa na Joseph Amon (23) .
 
 
Kashai  alisema  licha ya vifo hivyo,pia kuna majeruhi 22 wamelazwa katika hospitali ya kasulu na wawili   hali zao mbaya na hivyo  kuhamishiwa hospitali ya Heri Mission kwa matibabu zaidi  .huku akiri mwendo kasi chanzo cha ajali hiyo sambamba na   jitihada za kumkamata dereva wa Basi la Kambas zinaendelea.

No comments: