Balozi
wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada akiongea na waandishi wa habari
pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani) wakati wa
kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa
Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma. Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) nchini Yasunori
Onioshi akiahidi shirika lake kuendelea kushirikiana na Serilkali ya
Tanzania katika masuala mbalimbali yamaendeleo nchini, leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya waandishi wa habari pamoja, Maafisa kutoka Wizara ya Fedha na
Ubalozi wa Japani wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya
Salum wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali
ya Japani kwa Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma.
(Picha na habari na Ingiahedi Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara ya Fedha)
…………………………………………………………….
Wakati wizara ya fedha ikiendelea
na majadiliano ya Bajeti ya Serikali mjini Dodoma, Serikali ya Japan
imetoa kiasi cha Yen za Kijapani bilioni 1.5 ambazo ni sawa na shilingi
bilioni 24.1 za kitanzania kutoka Serikali ya Japani kwa ajili ya
shughuli za maendeleo hapa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo ya
kutiliana saini , Waziri Mkuya aliishukuru Serikali ya Japani kwa kuwa
na ushirikiano mzuri na Tanzania.
“Mkopo huu utachangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2014/2015, na fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Maji, Elimu na Afya” alisema Waziri Mkuya.
Aidha, Mkuya aliendelea kusema kuwa, “tunatoa shukurani kwa Serikali ya Japani kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa ambayo imeleta mafanikio makubwa nchini ambapo hivi sasa tumeona umaskini unapungua na kipato kinaongezeka kwa wananchi kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya watu na makazi ya 2012”.
Akijibu swali kuhusu fedha hizo za mikopo kuchelewa kufika, Waziri Mkuya alisema kuwa changamoto kubwa ambayo Serikali imekuwa ikiipata ni kutokana na taratibu za sera za nchi husika ambapo kila nchi wana sera zao.

Kwa upande wake Balozi wa Japan
Nchini Tanzania Masaki Okada alisema kuwa msaada huo unahusiana na
ushirikiano wa pamoja na Benki ya Dunia katika mkopo wa kumi na moja wa
kusaidia kupunguza umaskini ambao umekuwa ukitolewa tangu mwaka 2001.
Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa kwa masharti ya mkataba wa mkopo nafuu wa riba ya asilimia 0.01 kwa Serikali hapa nchini.
Balozi Okada alisema kuwa nchi
yake imekuwa ikitoa mikopo mabalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania
katika kupunguza umaskini ambapo misaada hiyo imekuwa ikitumika
kufuatana na GBS hapa Tanzanaia kwa kutoa fedha moja kwa moja ambazo
zinalenga kuharakisha juhudi za kupunguza umasikini hususani MKUKUTA.
Naye Mwakilishi wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) nchini Yasunori Onioshi alisema
kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na Serilkali ya Tanzania
katika kusaidia bajeti yake kwani Tanzania inakua kwa haraka na mahitaji
yake yanaendelea kuongezeka kila mara.
Makampuni ya Kijapani yanayofanya
kazi na Serikali ya Tanzania ni pamoja na Kampuni ya Sigara (TCC)
inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Tumbaku ya Kijapani, Panasonic
Energy Tanzania na JICA.
Hali ya hewa ya Dodoma ni baridi na majadiliano kuhusu Bajeti ya Serikali yameanza na yanaendelea.
Imetolewa na:
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
16/06/2014
No comments:
Post a Comment