Na Mwandishi wetu
Imeelezwa
kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo
ya kiserikali peke yao kufanya kazi hiyo
Kauli
hiyo imetolewa jana Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine
Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa
Afrika yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika
viwanja vya mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe
Hata
hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio
wengi Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira
magumu ambao wanahitaji msaada wa kila mmoja
“Ni
kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo
wilayani mwetu, hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya
uwezo wake, mwenye sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya
hivyo kwa wakati wake” amesema Matiro.
Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro(wa tatu kushoto walioketi) na
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba
(wa pili walioketi kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
shirika la wasaidizi wa kisheria Makete.
Katika
risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya
msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio
wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na
hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang’anya
misaada wanayopewa na wadau mbalimbali
Naye
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen
Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna
watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na
hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata
mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu
Hivyo
amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa
kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda
wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia
Katika
maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na
Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea
Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa na
kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa
taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua
za kisheria
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo”
Katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Iwawa Makete ambao nao walishiriki.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ndulamo wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha/habari na Edwin Moshi na Conrad Mpila, Makete).
No comments:
Post a Comment