Na Nathaniel Limu, Iramba
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la
mkoa wa Singida,linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 485 milioni
kugharamia utekelezaji wa mradi wa ‘Pamoja Tunaweza’ katika vijiji 62
vilivyopo kwenye kata 13, za wilaya ya Iramba na wilaya ya Mkalama.
Mradi
huo wa miaka mitano ambao unatarajiwa kumalizika mwakani,lengo lake ni
kuinua hali za afya za uzazi kwa akina mama na watoto.
Meneja
wa shirika la HAPA, David Mkanje, alisema hayo wakati akizungumza
kwenye hafla iliyofana ya makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya
shilingi 7.4 milioni vilivyotolewa na shirika hilo la HAPA,kwa kijiji
cha Mlandala kata ya Urughu wilaya ya Iramba.
Alisema
fedha hizo zilizotolewa na shirika la nchini Uholanzi la SIMAVI,
zinatumika katika kuhamasisha jamii kuhusu uzazi salama ambapo baba na
mama wanatakiwa kuhudhuria klinki pindi mama anapokuwa mjamzito.
“Pamoja
na ununuzi wa vifaa tiba na ujenzi wa majengo la kutolea huduma za
afya,pia tunatoa elimu kwa jamii kuhusu unyanyasaji wa akina mama pindi
wanapokuwa wajawazito na kuwapunguzia kazi,ili kulinda usalama wa mama
na mtoto”,alifafanua Mkanje.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mlandala kata Urughu wlaya ya Iramba,Mahona Mahela,
akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vya zanahati ya
kijiji hicho vilivyotolewa msaada na shirika la HAPA la mjini Singida.
Kulia ni meneja wa shirika la HAPA, David Mkanje.
Kuhusu vifaa vilivyotolewa kwa zahanati ya Mlandala, Meneja huyo alivitaja kuwa ni kitanda cha kujifungulia, tray ya kubebea dawa,vifaa vya uzalishaji,mizani ya watu wakubwa,mizani ya watoto na stendi ya dripu.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Iramba, Dk.Antony Mburu, alisema kuwa utafiti unaonyesha kuwa kijiji cha Mlandala chenye wanawake 168,ni wanawake chini ya kumi (10),ndio wanajifungulia kwenye zahanati ya kijiji hicho.
“Hii ni hatari,inaonyesha akina mama wengi wajawazito wanajifungulia nje ya vituo vya afya,jambo ambalo ni hatari kwao na watoto wao.Sasa HAPA imewapatia vifaa bora vya kujifungulia,nina imani kwamba akina mama wajawazito,sasa watakimbilia kujifungulia hapa kwa usalama wao na watoto wao”,alisema Dk.Mburu.
Wakati huo huo,muuguzi wa zahanati hiyo Sekela Michael, pamoja na kulishukuru shirika la HAPA,alisema zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la umeme.
Sekela alitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa usafiri katika kijiji hicho ambacho kipo umbali wa zaidi ya kilomita 100 kutoka ilipo hospitali ya wilaya.
Kaimu mganga mkuu wa
wilaya ya Iramba, Dk.Antony Mburu, akizungumza kwenye hafla ya
makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4
milioni vilivyotolewa msaada na shirika la HAPA.
Meneja wa shirika la
HAPA, David Mkanje (kushoto) akimkabidhi kaimu mganga mkuu wa wilaya ya
Iramba, Dk.Antony Mburu,mizani ya kupimia watoto wachanga,ambayo ni
sehemu ya msaada tiba wenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4 milioni
uliotolewa na HAPA.
Baadhi ya wageni
waliohudhuria hafla ya makabidhiano wa vifaa tiba vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi 7.4 milioni vilivyotolewa msaada kwa kijiji cha
Mlandala kata Urughu wilaya ya Iramba.(Picha zote na Nathaniel Limu).
No comments:
Post a Comment