Pages

KAPIPI TV

Monday, June 23, 2014

MTEVU AWAKINGIA KIFUA MAMALISHE DHIDI YA BOMOABOMOA TEMEKE

Abbas Mtemvu
Na Mwandishi Wetu
BOMOA Boboa ya vibanda vya mamalishe katika eneo la Viwanda la Mbozi, Temeke Dar es Salaam, limezua mtafaruku kufuatia mbunge wa jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu kuwakingia kifua mamalishe hao.

Pamoja na kuahidi kuchukua hatua ya kupambana kisheria na Halmashuri ya Jiji la Dar es Salaam, inayoendesha bomoa boboa hiyo, Mtemvu amewata mamalishe kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo.

"Jambo hili la kunyanyasa wananchi kwa kuwafukuza katika maeneo bila kufuata taratibu halikubaliki hata kidogo. Sasa mimi nawasaka watu hawa wa halimashauri ili kuzungumza nao, lakini wakati nafanyaa hivyo nawaagiza muwendelee na shughuli zenu hapa, na atakayekuja kuwafukuza mwambieni achukue kila kitu nami nitapambana naye kisheria", Mtemvu amesema hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya mamalishe hao katoka eneo la viwanda la Mbozi.

Mtemvu alisema, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hawakupaswa kuwafukuza mamalishe hao kwa kutumia mgambo kuvunja vunja vifaa na kuondoka na baadhi ya vyakula kama ambavyo imedaiwa, kwa sababu ujenzi wa barabara waliyopo hautarajiwi kufanywa hivi karibuni.

Amesema mbali na ujenzi wa barabara hiyo ambao Mtemvu alisema fedha za ujenzi amezitafuta yeye kama mbunge, pia ilipaswa mamalishe hao kutengenezewa mazingira mengine ya kuendelea na biashara zao kwa kuwa ni tengemeo kwa wafanyakazi kwenye viwanda vinavyozunguka eneo hilo.

Mtemvu alisema kutimuliwa bila kufanyiwa utaratibu mbadala, kutawafanya kinana mama, wasichana na vijana wanaojishughulisha na biashara hiyo ya mamalishe sasa kutafuta njia mbadala ya kuishi hata kama ni haramu jambo ambalo litakuwa siyo jema kwa taifa.

Juzi, Jiji kwa kutumia mgambo na tingatinga, walivamia eneo hilo la Mbozi na kusambaratisha vibanda vyote vya mamalishe waliopungua 35, na inadaiwa kwamba katika operesheni hiyo mgambo waliondoka na baadhi ya vyombo na vyakula ambavyo hadi sasa havijulikani vilipo.
 Mmoja wa Mamalishe eneo la Mtaa wa Viwanda la Mbozi, Temeke Dar es Salaam, Amina Saidi (kushoto) akilalamika mbele ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, mbunge huyo alipotembelea eneo la tukio kuona hali halisi leo mchana.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akitazama hali ilivyobaki baada ya bomoabomoa iliyofanywa na Jiji kwenye vibanda vya mamalishe katika mtaa wa Mbozi, Temeke.

No comments: