Msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni ambao bado unaendelea kuwepo kwa migogoro baina ya viongozi wa dini ambao pia umeambukiza waumini wa dini ya Kiislamu wa mjini Tabora. |
Katika hali ambayo haikutarajiwa na Waumini wa dini ya kiislamu mjini Tabora mgogoro huo sasa umeingia katika sura mpya na kusababisha hata kufanyika Ibada huku askari Polisi wakizunguuka maeneo ya msikiti huo ikidaiwa kulinda hali ya utulivu.
Hata hivyo aliyekuwa Sheikh Mkuu wa mkoa wa Tabora Shaaban Salum amejikuta akiwa mikononi mwa Polisi baada ya kudaiwa kumzuia kuendesha ibada Sheikh mkuu mteule Ibrahimu Mavumbi aliyeshika wadhifa huo kwa kuteuliwa na Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Simba kutokana na kupatikana na tuhuma za ubadhirifu katika msikiti huo mkuu wa Ijumaa Gongoni.
Shaaban Salum alidaiwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa msikiti huo kubadilisha nyaraka za umiliki kutoka kwa Baraza kuu la Waislamu nchini Bakwata kwenda kwa Waumini wa dini ya Kiislamu hatua amba imepingwa na jopo la Maulamaa linaloongozwa na Sheikh mkuu wa Tanzania na kupendekeza avuliwe madaraka kutokana na kadhia hiyo.
Baadhi ya waislamu waliowengi mkoani Tabora hawakuridhishwa na hatua aliyoichukua Mufti wa Tanzania kwa kumsimamisha kiongozi huyo Sahaban Salum anayekubalika na idadi kubwa ya Waumini wa dini ya kiislam mjini Tabora.
Kwaupande mwingine baadhi ya waislamu wamekuwa na hamu ya kumtaka Sheikh mkuu wa Tanzania kuwasikiliza maoni yao waislamu wa mkoani Tabora kabla ya kutoa uamuazi huo ambao wameendelea kuulani kila siku kwakuwa wanaamini Sheikh Shaaban Salum ameonewa kwakile walichodai kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kudhibiti mapato ya michango mbalimbali inayotolewa na Waumini wanaofanya ibada katika Msikiti huo.
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kuwashikilia kiongozi huyo wa dini ya kiislam mkoani Tabora pamoja na waumini wengine watano na kuwanyima dhamana kimeendelea kuibua hisia tofauti kwa baadhi ya waumini ya dini hiyo na kujijengea dhana kuwa ni shinikizo la baadhi ya viongozi wa Serikali mkoani Tabora kwa Jeshi la Polisi.
Mtandao huu umemtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda ili aweze kuzungumzia shutuma hizo za waislamu dhidi ya Polisi hakuweza kupatikana kwa nia ya kuzungumzia hilo.
No comments:
Post a Comment