Martha John katikati akiwa na
washindi wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya kutangazwa mshindi wa
taji la Redds Miss Iringa 2014 jana katika ukumbi wa St Dominic huku
mshindi wa pili ni Elizabeth Titus na mshindi wa tatu ni Fowe
Mkuchu(picha na Francis Godwin)
………………………………………………………………………………..
Na Francis Godwin blog, Iringa
MREMBO Martha John kuuwakilisha
mkoa wa Iringa katika mashindano ya Redds Miss kanda ya nyanda za
juu kusini baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redds Miss Iringa 2014
baada ya kuwashinda washiriki wenzake nane waliojitosa katika
kinyang’anyiro hicho .
Martha alitawazwa kuwa mrembo
wa mkoa wa Iringa jana usiku katika ukumbi wa St Dominic shindano
lililoshuhudia na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita .
Kutokana na ushindi huo Martha
kwa sasa ndie atakayeuwakilisha mkoa wa Iringa katika shindano la
kumsaka Redds Miss Kanda ya nyanda za juu ,onyesho linalotarajia
kufanyika ijumaa ya wiki ijayo mjini Iringa.
Jaji mkuu wa shindano hilo
Dosi Magambo mbali ya kumtangaza Martha kuwa mshindi wa kwanza
katika kinyang’anyiro hicho pia alimtangaza mshindi wa pili kuwa
ni Elizabeth Titus na mshindi wa tatu ni Fowe Mkuchu
Akikabidhi zawadi kwa
washindi hao kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bw Guninita alisema kuwa
ni imani yake na ya serikali ya Rais Dr Jakaya Kikwete kuona wasanii
na washiriki wa michezo mbali mbali wanaendelea kufanya vema katika
nafasi zao ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika sanaa mbali mbali.
Guninita alisema kuwa mrembo
huyo ambae ameshinda taji hilo ni lazima kuendelea kufanya vema
katika shindano la kanda na katika shindano la Taifa kama sehemu
ya kuuwezesha mkoa wa Iringa kufanya vema zaidi na ikiwezekana
Redds Miss Tamzania kutoka mkoa wa Iringa.
Awali Redds Miss Iringa 2013 Neema Mality alimtaka mrithi wake kujitahidi kujiheshimu na kutunza heshima ya taji hilo .
Shindano hilo lililoandaliwa
na kituo cha Radio Nuru Fm chini ya uratibu wa Victor Chakudika
washiriki wote walipewa kifuta jasho cha Sh. 100,000 wakati mshindi
wa kwanza alizawadiwa kiasi cha Tsh 500,000 , mshindi wa pili Tsh
300,000 na mshindi wa tatu aliambulia kiasi cha Tsh 200,000
No comments:
Post a Comment