Kamishna
wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akisalimiana
na Maafisa Waandamizi wa Magereza Mkoani Kilimanjaro alipotembelea
Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014 Mkoani
Kilimanjaro. Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Rafael Tuhaferi(wa pili kushoto)
akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Kiwanda cha viatu,
Gereza Karanga Moshi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa. Wafungwa
wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakishona viatu vya ngozi katika Kiwanda
cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Wafungwa hao wamepewa Mafunzo ya
Ufundi wa kutengeneza viatu vya aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa ambapo
kutokana na ujuzi huo pindi wamalizapo vifungo vyao watakuwa wamepata
ujuzi ambao utawasaidia huko katika jamii zao. Viatu
aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi
na Usalama hapa Nchini vinavyotengenezwa na Kiwanda cha Viatu, Gereza
Kuu Karanga Moshi. Kiwanda hicho pia hutengeneza viatu vya ngozi vya
aina mbalimbali ambavyo hutumiwa pia hata na raia. Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi)
akiteta jambo na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(vazi la drafti) alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu
Karanga Moshi, Juni 21, 2014. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza Mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment