Na Magreth Magosso, Babati.
WITO umetolewa kwa madereva wa vyombo vya moto vya usafiri wa Barabarani kuwa makini na matumizi bora ya barabara hasa maeneo ya mapito ya wanyama , ili kuepusha vifo vyao kwa kuwagonga na magari na hivyo kuhatarisha
kutoweka kwa baadhi ya wanyama kwenye hifadhi za taifa.
Akithibitisha kauli
hiyo Mhifadhi wa Ekolojia hifadhi ya Tarangire Abel Peter alisema wanyama wapo hatarini kutoweka, kutokana tabia
ya baadhi ya madereva hasa wa malori makubwa kutozingatia
sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo vya wanyama pindi wavukapo ng`ambo ya pili ya barabara ya babati-manyara.
“Wanyama aina ya Fisi miraba, chui, Simba hasa jamii ya paka na
mbwa mwitu wapo hatarini kutoweka
kutokana na vifo vitokanavyo na ajali ukizingatia wapo wachache na uzao wao ni
wapolepole” alifafanua David Maige ambaye ni mhifadhi utalii.
Tabia ya mwendo kasi
inachangia serikali na shirika la hifadhi kutoboresha miundombinu ya barabara
kwa kiwango cha lami zilizo karibu na hifadhi kwa kuhofia ongezeko la vifo vya
wanyama wanaohamahama hupoteza maisha
katika vivuko vyao.
Takwimu zinaonyesha
idadi ya wanyama aina ya Simba wamepungua kutoka 400 katika kipindi cha mwaka
1990 hadi kufikia 120 kwa mwaka 2013/2014ambapo inachangiwa na sababu
mbalimbali ikiwemo jamii kuwauwa pamoja na ajali za barabarani.
Hata hivyo hifadhi imejipanga
kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii,
kushiriki maonyesho, kushirikiana na waandishi wa habari kutoka kwenye maeneo
mbalimbali ili kutangaza na kufichua uhalifu uliopo katika hifadhi jambo
litakalosaidia kutatua changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment