Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Henry Kapufi wakisikiliza maelekezo juu ya
ufugaji nyuki kutoka kwa mmoja wa wafugaji(hayupo pichani) katika
kijiji cha mabilioni wilayani Same katika siku ya kupambana na kuenea
kwa hali ya jangwa na ukame duniani Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipanda mti
wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali
ya jangwa duniani zilizofanyika katika kijiji cha mabilioni wiayani
Same.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akiongea na wananchi katika maadhimisho hayo . Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya msanja sanjari na kikundi cha wakinamama wa kijiji cha mabilioni wilayani Same katika maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akiongea na wananchi katika maadhimisho hayo . Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya msanja sanjari na kikundi cha wakinamama wa kijiji cha mabilioni wilayani Same katika maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akihutubia
katika siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Kitaifa maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika katika kijiji cha
mabilioni Tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
……………………………………………………………………
Wito umetolewa na Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwaimu kwa jamii ya Umma wa
Tanzania kutunza ardhi na udongo kwa ajili ya matumizi endelevu na
kuifanya ardhi iwe na uwezo wa kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo na
kutoa huduma zingine muhimu ili kuepuka hali ya jangwa na ukame kwa
kizazi cha sasa na kijacho na pia kuchukua hatua madhubuti za
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mheshimiwa Mwalimu amesema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho
ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika kijiji cha Mabilioni tarafa
ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
Aliongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa robo ya dunia ambayo ni
zaidi ya hekta bilioni 3.6 inatishiwa na janga la kuenea kwa hali ya
ukame na jangwa. Hivyo basi alisema ni wajibu wa kila mmoja kulinda
ardhi ili iweze kuleta manufaa baadaye sababu kuenea kwa hali ya jangwa
na ukame kunasababisha matatizo ya kiuchumi,kimazingira na kijamii .
Vivyo hivyo kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunapelekea ardhi
kupunguza uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula na kuongeza umaskini .
Mwisho alitoa wito kwa Hamashauri zote Nchini kuunda kamati za
Mazingira kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Wilaya. Pia aliomba vyombo vya
habari Nchini kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu
wa kuchukua njia thabiti za kupambana na kuzuia kuenea kwa hali ya
jangwa na ukame.Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Ardhi ni mustakabali
wa maisha, tuilinde dhidi ya uharibifu.
No comments:
Post a Comment