Bibi mmoja anayefahamika kwa jina la Sada Issa Muduta(70)mkazi wa Kijiji cha Usungu Kata ya Ndono wilaya ya Uyui mkoani Tabora amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete baada ya kubakwa na mtoto wake ambaye anafahamika kwa jina la Sizya Mgaya....Tukio hilo ambalo lilitokea mnamo tarehe 22 juni mwaka huu majira ya saa nane usiku ambapo imeelezwa kuwa Kikongwe huyo Bibi Sada akiwa nyumbani kwake amelala mtoto wake Sizya Mgaya alimnyatia baada ya kuingia chumbani alikokuwa amelala na kuanza kumbaka baada ya kumpa kipigo licha ya kuwa kikongwe huyo alipiga kelele ya kutaka msaada lakini haikuwa rahisi huku Sikzya akipata mwanya wa kuendelea kutekeleza unyama huo kwa mama yake mzazi hali iliyosababisha kupoteza fahamu kwa bi mkubwa huyo wakati akifanyiwa kitendo hicho cha fedheha.....Hata hivyo Jeshi la polisi linamshikilia Sizya kwa madai ya kuhusika na unyama huo dhidi ya mama yake mzazi. | |
No comments:
Post a Comment