Katika hali ambayo imewashangaza wengi mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora,baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kanda ya Magharibi wamekuwa wakipitapita mitaani na kuwahamasisha watu wajiunge na chama kipya cha ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT).
Viongozi hao ambao wengine walikutwa wakiwa wamevalia sare za Chadema wamekuwa hata wakiwataka wanachama wa Chadema kukihama Chama hicho huku wakidai kuwa Chadema kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa madaraka na tena matumizi mabaya ya rasilimali wakipigia mfano rasilimali fedha zilizotumika katika chaguzi ndogo zilizopita hivi karibuni.
Hata hivyo viongozi hao ambao wamekuwa hawaweki bayana kitendo cha kuhamasisha watu kujiunga na ACT wakati wao wamevalia sare za Chadema mbali na kuonekana wasaliti lakini wamekuwa wakijitetea kwa madai ACT ndio chama pekee chenye uchungu na wananchi na kwamba kitaendelea kujali maslahi ya umma kwanza licha ya kuwa bado ni chama kipya.
Pamoja na kuelezea madhaifu makubwa yanayofanywa na viongozi wa Chadema ngazi ya juu,viongozi hao ambao kwasasa imedaiwa wametoweka katika mikoa yao na kwenda jijini Dar-es-salaam ambako kazi ya kuendelea kukiimarisha ACT inaendelea kwa kasi inasemekana hivi karibuni watarudi katika mikoa yao iliyopo kanda ya Magharibi na kutangaza rasmi kuwa tayari wamejiunga na ACT ambayo itakuwa tayari kukabiliana na Chadema kwenye chaguzi mbalimbali zijazo huku wakitarajia kuifuta kabisa Chadema kanda ya magharibi.
No comments:
Post a Comment