ADY
de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta
mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani
Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY
de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo
nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na
kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome Kongwe
kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka
kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la
Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada
anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong’aa majira ya
magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa
anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na Kulia
rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake
Nautenle Batista.
Alipokewa
na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo
kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha
kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika
ukumbi wa sinema.
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia.
Kabla
ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na Júlio Mesquita,
mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ângelo Torres na Ciomara Morais,
Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia,
anashukuru sana.
Sinema
hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya
maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo
imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.
ADY de Batista akizungumzia filamu yake.
Maneno
ya ndoto kutimia yameonesha furaha aliyoiandika katika mtandao wa
kijamii wa Facebook Mei mwaka huu baada ya kuambiwa kwamba filamu yake
imeingia katika mashindano ZIFF.
Katika
hiyo face book ya Mei mwaka huu aliandika: E nós fomos seleccionados!
Júlio Mesquita Audilia Batista Daniel Martinho Daniel Martinho Angelo
Torres Ciomara Morais Sonia Claudia Neves Eric Santos Eric Santos
akimaananisha : Tumechaguliwa! akiwataarifu Júlio Mesquita Audilia
Batista Daniel Martin Daniel Martin Angelo Torres Noelle Matthews Sonia
Santos Santos Eric Eric Claudia Neves .
Shangilio
lililokuwa katika facebook ndilo hasa alilolionesha wakati akizungumzia
sinema yake hiyo ambayo ilipigwa picha kwa siku 20 na kutoa matokeo
kama sinema ya Hollywood kwa ubora.
Ikiwa
inajulikana kama The Thorn of the Rose,kwa kingereza, filamu hii ambayo
ilikuwa ya kwanza kwa mtengeneza sinema Filipe Henriques ipo katika
maelezo ya ushindani ambayo yanatoa ubora wa picha na skripti yenyewe
kwa namna ambavyo matukio yamefungwa pamoja na kuwa kama visa zaidi ya
viwili katika filamu.
Kiukweli
wakati natazama sinema hii Ngome Kongwe na hata katika maonesho binafsi
ya ndani ya ukumbi wa kujitegemea Double Tree Hotel, ina wakati
inakuchanganya mwenendo ambao unatakiwa kuwa nao makini kwani kuna muda
unajisikia kama kutapika kwa hasira wakati mtengeneza sinema alipokuwa
akiiperemba jamii na makovu ya wanasiasa.
Unaweza
kusema kwamba simulizi hili lina mashetani, lakini masimulzii yake
yanakupa neno jema kabisa la kuzungumza wakati ukimaliza kuona sinema
hii.
Mwendesha
mashtaka David Lungha (Júlio Mesquita) katika filamu hii anakutana na
binti mrembo ambaye uwepo na utokeaji wake ni wa ‘utata’ zaidi
anayekwenda kwa jina la Rosa (Ady Batista).
Hawa
wawili wanakutana katika baa ambapo watu walikuwa wanamsubiri kumpa
hongera kwa ushindi wake mahakamani. Amabo anaukiri na kusema mapambano
yanaendelea.
Akisema hivyo anakwenda kukaa katika kiti cha baa na pembeni mwake kuna askari polisi.
Akiketi
pale mmoja wa wasaidizi wake anafika kwake akionekana wazi si tu kutoa
hongera bali kumtaka kimapenzi na kumkataa, lakini akiondoka analetewa
bahasha na mtandia , lakini kabla ya hapo anazungumza na polisi ambaye
anamwambia hakuna ua waridi lisilokuwa na miba na ogopa unapopata ua
waridi tatu.
Akaondoka akmfyonza lakini kweli aliona kuna ua waridi na maneno ya polisi yanaweza kuwa kweli.
Muda
mfupi tunasikia kishindo cha kiatu na anaingia binti wa kike ambaye
mwendesha mashtaka anaingiwa na kwikwi na wanaanza mambo ambayo
yanapeleka katika mtandao mkubwa zaidi wa uwongo, kusalitiana, mauaji na
rushwa.
Ukiangalia
sinema hii hata mwanzo unapata maswali mengi kama kweli Rosa ni mtu
kweli au ni mawazo ya mwendesha mashtaka, ama ni mzimu ambao hauwezi
kutulia kuzimu mpaka habari ya kifo chake ielezwe.
katika
simulizi hili muigizaji kinara David Lungha ni mwanamume mwenye mvuto
mkubwa wa kimapenzi lakini mtata; na mtu wetu wa leo katika sebule la
sinema Ady Batista ni mdada mzuri, ambaye anaonekana kuchukua kiatu cha
Rosa, kama asiyekuwa na raha huko aliko.
Ndani humu Eric Santos ni askari ambaye amekuwa polisi akiwa na siri nyingi mbaya za kwake.
Lakini
msimuliaji wetu anataka kukueleza kwamba si sahihi kuacha kurekebisha
mambo na wale waliokufa, kwani hutafuta njia ya kurudi na kurekebisha
mambo yao, imani ambayo Waguinea wanayo sana.
Mapenzi
ya mwendesha mashtaka David Lunga kwa Rosa kuna vuruga kila kitu na
Lunga anajikuta akifanya vitu vingi kwanza kumaananisha kwamba hana kosa
wala hana sababu ya kujuta.
Filamu
hii ambayo iliwapa shida watu wa sensa wa ZIFF ili iweze kuonwa na watu
wengi ukumbi wa wazi, unazungumzia kwa namna ya pekee rushwa, ubakaji
ambao unafanywa katika maisha ya binti, kifo chake na jinsi ambavyo
anataka jumuiya ijue.
Pamoja
na kwamba binti alikufa katika utata wa kutoa mimba alirejea duniani
kutafuta msaada wa haki kutendeka na katika hili Polisi yule (askari wa
zamani) aliwaua lakini akashindwa kummaliza moja kwa moja Lunga ambaye
alimuua.
Kiukweli kuelekea mwisho wa sinema unaona matukio mengi na jinsi hali ilivyo ngumu na lazima aifanyie kazi.
Filipe
Henriques ameifanyakazi kubwa sinema hii ambayo imejaa usaliti kuanzia
wa kisiasa, kijamii hadi kimapenzi huku mazungumzo yakiwa mapenzi kwa
watoto wadogo.
Lugha
ya kireno ambayo imeambatana na lugha ya kiingereza katika maandishi
yanayopita si nzuri kihivyo, lugha ina matusi mengi na isiyopendeza na
kuna grafiki za mapenzi ya kulazimishwa katika hali isiyokubalika.
ADY de Batista akiondoka mara baada ya kumalizika kwa filamu yake.
Mdada
huyu ambaye katika mazungumzo alisema kwamba simulizi la sinema ile ni
matukio ya kweli nyumbani kwao ambapo pia kuna imani kubwa kuhusu mizimu
kurejea duniani pamoja na kuwapo dini ya Kikristo na Kiislamu,ametaka
jamii kujipambanua na maradhi ya woga na kuchukua hatua kwanza binafsi
na kisha kijamii dhidi ya maovu.
Mdada huyu ambaye hajaolewa lakini ana rafiki wa kiume, alikuwa Zanzibar na mdogo wake na Meneja wake.
Mdogo wake ndiye anayejua kiingereza kwa ufasaha zaidi huku yeye mwenyewe amebahatisha.
Nilipomuuliza kuhusu nguo yake nyeupe, kwani katika sinema kuna vazi la harusi, alisema rangi nyeupe ni alama ya matumaini.
Kuendelea kusoma zaidi bofya hapa
No comments:
Post a Comment