Pages

KAPIPI TV

Thursday, May 1, 2014

MVUVI AWAPIGA BAO MAJAMBAZI KIGOMA

WAKAZI  wa Manispaa ya kigoma Ujiji,wamempongeza mvuvi Jerome Sambulumaa kwa kitendo chake cha  kurudi na mashine 4  za mitumbwi kati ya 9  zilizoibwa  Ziwa Tanganyika  Aprili, 29,2014 na  majambazi watatu raia kutoka DRC-Congo .

Pia wavuvi wamemtaka  Rais Jakaya Kikwete  aingilie kati kilio cha wavuvi mkoani hapa na si kuiachia kamati ya ulinzi ya mkoa huo sanjari na kutovitegemea vikao vya ujirani mwema ambavyo havina tija ya changamoto hiyo baina ya nchi hizo.

Akielezea tukio hilo kiongozi wa wavuvi Francis John alisema  Aprili,29 saa 5 usiku walipewa tarifa ya uvamizi huo ziwani na baadhi ya wavuvi walioporwa mashine katika mwalo wa kibirizi na katonga.

Alisema Aprili 30,2014 walipokea simu kutoka kwa mvuvi huyo akiwambia yupo njiani kuja kigoma ila alipungukiwa na mafuta katika mtumbwi wake,ndipo walienda na wadau wengine na kumsaidia hadi kufika kigoma  siku ya Mei mosi saa 5.45 asubuhi.

Akifafanua matukio ya ujambazi ziwa Tanganyika Mwenyekiti wa wavuvi  kigoma Ramadhan Kanyongo alisema mwalo wa kibirizi wameiba mashine 5 na kibirizi  mashine 3  na kudai changamoto hiyo ni udhaifu wa kamati ya ulinzi.

“ acha nikupe siri ,doria ya majini ipo lubengela sasa tukio limetokea  jumanne saa 5 usiku na tarifa ilipelekwa kwa Kamanda usiku huohuo,cha kushangaza jumatano saa 7 mchana ndio wanakwenda kuwatafuta majambazi , askari hawalali saiti wanatafutana baada ya janga udhaifu upo wapi” alihoji Kanyongo.

Alisema mto Lukuga upo karibu na kambi ya jeshi wilaya ya Kalemii,na majambazi wanatumia eneo hilo kuvusha zana za wizi kutoka hapa,ambapo zaidi ya bilioni 7 za mali za wavuvi  kigoma zimepotelea nchini humo.huku akimtaka Rais Jakaya aingilie kati suala hilo ambalo ni chachu ya vurugu nchini.

Naye mhanga wa mashine hizo Ally Mzila alisema Jerome ni kijana wake,amefanya tukio la kishujaa kuokoa injini za mashine za mitumbwi minne kati ya tatu zilizochukuliwa na wahalifu hao.

Baadhi ya kina mama wenye watoto wao wanaojishughulisha na uvuvi ziwani humo Amina Said,Mwaija Juma na Vumilia Ismaili kwa nyakati tofauti walisema wanahofia usalama wa vijana wao ziwani,kutokana na matukio ya uvamizi ziwani kushamiri kila mwezi.

Kwa upande wa RCO wa mkoani hapa Dismas Kisusi alipoulizwa kuhusu hili,akiri kutokea na kuwambia wandishi wa habari wasubiri kesho wataitwa na Kamanda wa mkoa Frasser Kashai ambaye alikuwa wilayani Uvinza kwenye madhimisho ya Meimosi.huku Balozi mdogo wa DRC-Congo alidai anafanya mawasiliano na mkuu wa wilaya ya kalemi kubaini hilo.

Pia katika mtubwi uliotumiwa na majambazi hao ambao pia mvuvi huyo alirudi nao ilikutwa simu ambayo inasadikiwa ilikuwa ikitumiwa na wahalifu hao siku mbili wakati wakiwa ziwani.

Aidha simu hiyo ikitumiwa vyema na kwa usahihi itakuwa nyenzo sahihi ya kubaini mtandao wa ujambazi katika ziwa hilo,gazeti hili linaamini endapo wizara husika ikichelea na kilio cha wavuvi kigoma  wakazi wa hapa hatarini kujingiza kwenye  matukio ya kihalifu kutokana na kukosa ajira.

No comments: