WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma wametakiwa wafanye usafi wa mazingira maradufu katika kaya zao ili waepukane na ugonjwa wa Dengue,ambapo kwa sasa mkazi mmoja amekutwa na ugonjwa huo.
Akifafanua kauli hiyo Mganga wa Mkoa Leonard Subi kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa alisema, kwa sasa kuna mgonjwa mmoja wilaya ya Buhigwe na anapatiwa matibabu katika hospitali ya misheni ya Heru,baada ya kuambuki zwa kirusi cha mmbu aina ya Edesi ambaye anaambukiza ugonjwa huo.
Alisema awali mkazi huyo alitoka jijini Dar-es-salaam na kuja hapa kwa lengo la kusalimia jamaa zake ndipo akapatwa na homa ya ghafla na baada ya kuchukuliwa vipimo vyote akagundulika na ugonjwa wa dengue.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya aliwaonya wananchi waache kupokea taarifa zisizo na utafiti wa uhakiki toka wizara husika juu ya tiba zinazotolewa katika mitandao ya kijamii kwa kubainisha tiba feki ya ugonjwa huo.
Alisema jamii ikubali maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya dalili husika hasa ya kutoka damu sehemu za wazi,kuchoka kwa viungo vya mwili,na waende kwenye vituo vya afya kwa uchunguzi zaidi kabla mgonjwa ajazidiwa.
N aye Katibu tawala wa mkoani hapa,Eng.John Ndunguru alisema bora kinga kuliko tiba,usafi unaondoa magonjwa kwa asilimia 55,hivyo jamii haina budi kuzingatia utunzaji na usafi wa mazingira kwa manufaa yao na mkoa kwa ujumla lengo kuepukana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo dengue.



No comments:
Post a Comment