Pages

KAPIPI TV

Wednesday, April 23, 2014

WANAFUNZI WAKOSA MASOMO KISA UHABA WA MADARASA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
 
Shule ya Sekondari kata ya Kajana iliyopo Wilaya ya Buhingwe Mkoani Kigoma, imeshindwa kupokea wanafunzi 70 waliotakiwa wajiunge na kidato cha kwanza kutokana na ufinyu wa vyumba vya madarasa.
 
 
Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 115 wa kidato cha pili na cha tatu kwa mwaka huu bado imelazimika kutopokea wanafunzi 70 waliotakiwa kuanza kiadto cha kwanza kwa mwa 2014 na hivyo kulazimika kuwapeleka katika shule ya tarafa hiyo.
 
Naye Mkuu wa shule hiyo Daudi Shipande alisema baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa wamelazimika kubaki majumbani kwao kutokana na kushindwa kukidhi mahitaji ya kujiunga na shule ya Sekondari Muyama ikiwa ni pamoja na umbali uliopo.
 
Alisema Shule hiyo ina nyumba vitatu vya madarasa ambapo vyumba viwili vinatumika kwa wanafunzi wa kidato cha pili na cha tatu na chumba kimoja kinatumika kama ofisi ya walimu pamoja na Mkuu wa Shule.
 
Ofisa Elimu Wilaya hiyo alisema  changamoto  hiyo ni pamoja na uchache vitendea kazi, ambapo walimu hawana meza na viti vya kukalia hivyo hulazimika kutumia viti vya wanafunzi na meza moja hutumiwa na walimu watatu.
 
 Leanda Johakimu mwanafunzi aliyepangiwa katika shule ya Sekondali Muyama alisema, kutokana nachangamoto hiyo itamlazimu apange chumba uraiani ili kukabiliana na shule zilizo mbali na shule hiyo ambayo imeshindwa kuwapokea.
 
 Mkuu wa Shule hiyo amewaomba wakazi wa Kijiji hicho kutambua kuchangia  ujenzi wa shule hiyo ni kwa manufaa ya vizazi vya leo na kesho hivyo washirikiane ili kuhakikisha ujenzi wa vyumba hivyo unakamilika

No comments: