Nembo ya Bohari ya Dawa (MSD)
Ofisa
Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam,
Florida Sianga (wa pili kulia), akiwaelekeza jambo waandishi wa habari
waliotembelea banda la MSD katika maonesho ya Siku ya Malaria Duniani
yaliyofanyika Kitaifa Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.Waliokaa kutoka
kushoto ni Balozi wa malaria wa MSD, Lameck Kipiliango na Ofisa
Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.
Ofisa
Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam,
Florida Sianga (wa pili kulia), akiwaelekeza jambo waandishi wa habari
waliotembelea banda la MSD katika maonesho ya Siku ya Malaria Duniani
yaliyofanyika Kitaifa Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.Waliokaa kutoka
kushoto ni Balozi wa malaria wa MSD, Lameck Kipiliango na Ofisa
Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.
Balozi
wa Malaria wa MSD, Lameck Kipiliango (kushoto), akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani), waliotembelea banda la MSD. Kulia ni Ofisa
Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.
Maofisa
wa MSD wakipanga bidhaa zao katika banda lao kwenye maonesho hayo.
Kutoka kushoto ni Ofisa Habari wa MSD, Etty Kusiluka, Balozi wa Malaria wa MSD, Lameck Kipiliango, Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid na Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam, Florida Sianga
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
PAMOJA
na kuwepo kwa malalamiko ya kukosekana kwa dawa za malaria katika
Hospitali mbalimbali hapa nchini Bohari ya Dawa (MSD), imesema ina dawa
za kutosha.
Hayo
yalibainishwa na Balozi wa Malaria wa MSD, Lameck Kipiliango wakati
akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la MSD katika
maonesho ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani, ambayo kitaifa
yamefanyika katika Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.
Akifafanua
zaidi, Kipiliango alisema wamekuwa wakishindwa kuweka makisio ya kiasi
cha dawa wanachohitaji na hivyo kujikuta zikiwaishia kabla ya muda na
hivyo kuonekana kama kuna upungufu kwa nchi nzima jambo ambalo sio la
kweli.
Kuhusu
MSD kuchaguliwa kama balozi wa malaria tangu mwaka jana, alisema
wamekuwa wakitelekeza shughuli mbalimbali ikiwemo mafunzo ya mara kwa
mara kwa wafanyakazi wao kuhusu ugonjwa huo.
Kama
vile haitoshi alisema wamekuwa wakimpatia kila mfanyakazi chandarua
kulingana na idadi ya familia yake kwa nia ya kuielimisha jamii
inayowazunguka umuhimu wa kutumia chandarua katika kujikinga na malaria.
Aidha kupitia wafanyakazi wao wamekuwa wakitoa elimu kupitia kanda tano walizozigawa katika maeneo mbalimbali nchini.
Naye
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es
Salaam, Florida Siyanga , alizitaja baadhi ya changamoto ambazo
wamekuwa wakikabiliana nazo katika usambazaji wa dawa ni uhaba wa
magari na ubovu wa miundombinu ambapo katika maeneo mengine wanalazimika
kutumia kutumia pikipiki au mitumbwi.
Katika
kutatua kasoro hizo, wito wake Siyanga alitaka watumishi kupata mafunzo
ya namna ya kuagiza dawa ili ziweze kuwatosha katika msimu mzima wa
mwaka ili wananchi wazipate kwa wakati.
No comments:
Post a Comment